Nenda kwa yaliyomo

Anton Praetorius

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Anton Praetorius ( Lippstadt, Ujerumani, 1560Laudenbach an der Bergstrasse, 6 Desemba 1613), alikuwa mchungaji wa Kiprotestanti.

Alikuwa mwanateolojia katika kanisa la John Calvini. Tena alikuwa mwandishi wa vitabu.

Alipiga vita ile desturi mbaya ya kushtaki watu fulani barazani hivi tu kuwa wachawi. Vilevile alipiga vita ili mateso ya wale walioshtakiwa yaondolewe.

Lippstadt
Pipa kubwa la Heidelberg
Wachawi wanaunguzwa
  • 1597 Praetorius alileta udaku mkali barazani ili kupinga mateso ya mama fulani aliposhtakiwa kuwa mchawi. Hakimu hakuendelea kumshtaki yule mama akafunga shauri. Mama huyo aliachishwa huru. Lakini Praetorius aliachishwa kazi yake kama mchungaji wa pale.
Laudenbach/Bergstrasse: Nyumba ya mchungaji
  • 1598 Praetorius alipata kuwa mchungaji wa usharika wa Laudenbach/Bergstrasse. Aliandika kitabu Ripoti juu ya Uchawi na Wachawi. Katika kitabu hicho alileta udaku ili iondolewe ile desturi mbaya ya kuwaonea watu kuwa wachawi, tena yaondolewe mateso. Alikiandika kitabu hicho akitumia jina la fumbo Yohana Scultetus lililokuwa jina la mwanawe.
  • 1602 na 1613 alikichapa kitabu chake tena, lakini mara hii alitumia jina lake la kweli. Toleo la pili 1602, la tatu 1613.
  • 1629 yeye alipokuwa amekwisha kufa toleo la nne la kitabu chake Ripoti juu ya Uchawi na Wachawi lilichapwa.
Ukurasa wa kwanza wa Ripoti ya 1602

.

Vitabu vya Anton Praetorius

[hariri | hariri chanzo]
  • De pii magistratus officio, iure ac potestate in religione et ecclesiis ad verbi Dei normam reformandis, 1596
  • Gründlicher Bericht von Zauberey und Zauberern per "Ioannem Scultetum Westphalo-camensem", 1598 (Kitabu cha kupinga uoneaji wa wachawi na mateso)
  • De sacrosanctis novi foederis Iesus Christi Sacramentis, 1602

Vitabu viliyotumika

[hariri | hariri chanzo]
  • Hartmut Hegeler: Anton Praetorius, Kämpfer gegen Hexenprozesse und Folter. Unna 2002, ISBN 3980896943 (Kitabu cha Hartmut Hegeler juu ya maisha ya Anton Praetorius aliyepiga vita uoneaji wa wachawi na mateso yao)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]