Anna Makinda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Anne Semamba Makinda)
Anna Makinda

Anna Semamba Makinda (amezaliwa 15 Julai 1949) alikuwa mbunge wa jimbo la Njombe Kusini katika bunge la taifa nchini Tanzania.[1] Pia alikuwa Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2006 hadi 2010. Alikuwa Spika wa kwanza mwanamke katika Bunge la Tanzania. Tangu mwaka 1990 hadi 1995 alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Pia miaka ya nyuma alishawahi kushika nyadhifa kadha wa kadha.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Mengi kuhusu Anna Makinda". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-19. Iliwekwa mnamo 2010-11-12. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Anna Makinda kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.