Adam Smith

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Adam Smith
Inquiry into the nature and causes of the wealth of nations, 1922

Adam Smith (16 Juni, 1723 - 17 Julai, 1790) alikuwa mwanafalsafa nchini Uskoti aliyeweka misingi kwa Sayansi ya Uchumi ya isasa.

Katika kitabu chake "Uchunguzi juu ya utajiri wa mataifa" (An Inquiry into the Nature and Causes of the Wealth of Nations) alieleza ya kwamba kama kila mtu ana nafasi ya kufuatilia faida yake ya binafsi ni afadhali kwa maendeleo ya taifa lote. Aliona njia hii kuwa afadhali kuliko serikali kupanga mambo ya uchumi kwa sababu kila mtu anajua mwenyewe mahitaji na uwezo wake. Aliona ya kwamba

Aliona ya kwamba msingi wa uchumi ni kazi ya watu inayoongeza thamani ya maliasili na arhi yenyewe. Kila mtu ana uwezo wa pekee na nafasi za pekee hivyo watu wanaelekea kuchagua sehemu ya nafasi zilizopo. Hii ni msingi wa ugawaji wa kazi mbalimbali kati ya watu. Nafasi ya kubadilishana mazao ya kazi kwenye soko huria inaleta matokeo bora kwa watu wote.

Nadharia hii imekuwa msingi wa falsafa ya ubepari lakini pia Karl Marx alitumia matokeo ya utafiti wa Smith kwa nadharia zake za usoshalisti.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]