ABBA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
ABBA
ABBA wakiwa na mwigizaji filamu Robert Hughes katika filamu ya ABBA. (Kutoka kushoto-kulia: Andersson, Ulvaeus, Fältskog, Hughes, na Lyngstad.)
ABBA wakiwa na mwigizaji filamu Robert Hughes katika filamu ya ABBA. (Kutoka kushoto-kulia: Andersson, Ulvaeus, Fältskog, Hughes, na Lyngstad.)
Jina la kisanii ABBA
Nchi Uswidi
Aina ya muziki Pop
Europop
Disco
Rock
Roll
Miaka ya kazi 1972 – 1982
Ameshirikiana na Hep Stars
Hootenanny Singers
Benny Anderssons Orkester
A*Teens
Björn Again
Kampuni Polar
Polydor
Atlantic
RCA
Universal
PolyGram
Epic
Carnaby
Sunshine
Ariston/Dig It
Vogue
Discomate
Philips

ABBA lilikuwa kundi la muziki wa aina ya pop kutoka nchini Uswidi, ambao waliwika sana kunako miaka ya 1970 na 1980. Jina la "ABBA" lilitokana na kila herufi ya kwanza ya jina la mwanakundi:

  • Agnetha Fältskog
  • Björn Ulvaeus
  • Benny Andersson, na
  • Anni-Frid Lyngstad.

ABBA walikuja kuwa maarufu sana baada ya kushinda mwaka 1974 katika mashindano ya kutafuta nyimbo bora za nchi za Ulaya (Eurovision Song Contest). Walikuwa na vibao vingi tu malidhawa. Vibao kama vile "Dancing Queen", "SOS", "Mamma Mia", na "Waterloo". Karibuni nyimbo zao zote zilikuwa zikitungwa na Ulvaeus na Andersson.

Kundi lilikuwa kuvunjika mnamo mwaka wa 1982, lakini bado vibao viliendelea kuwa maarufu. Nyimbo moja ya ABBA ilibahatika kuonekana katika baadhi ya filamu (ikiwemo filamu ya Kiaustralia-The Adventures of Priscilla, Queen of the Desert na Muriel's Wedding.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]