Stockholm

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kitovu cha kale cha Stockholm
Ramani ya Stockholm

Stockholm (pia Stokolimi) ni mji mkuu wa Uswidi na pia mji mkubwa wa nchi hito wenye wakazi 864,324 (31 Desemba 2011) ambao pamoja na rundiko la mji ni watu milioni 1.3.

Mji uko kwenye pwani ya mashariki ya Uswidi ambako ziwa Mälaren lajiunga na Bahari Baltiki. Kitovu cha mji ni visiwa 14 vinavyotengwa na mifereji yenye madaraja.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Birger Jarl alianzisha Stockholm mnamo mwaka 1252 BK kama boma la kuzuia maharamia wasiingie kwenye ziwa Mälaren na kushambulia miji huko. Mji ulianza kukua karibu na boma lile ukawa mji wa biashara katika shirikisho la Hanse.

Stockholm ilikuwa mji mkubwa lakini si bado mji mkuu kwa sababu wafalme hawakukaa mahali pa kudumu. Gustav Vasa alianzisha makazi ya wafalme mjini.

Makala hii kuhusu maeneo ya Uswidi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Stockholm kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.