Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Translated from http://en.wikipedia.org/wiki/Fertility_awareness (revision: 384592908) using http://translate.google.com/toolkit with about 96% human translations.
(Hakuna tofauti)

Pitio la 22:34, 30 Novemba 2010

Fertility awareness
Background
Birth control typeBehavioral
First use1950s (mucus)
mid-1930s (BBT)
1930 (Knaus-Ogino)
Ancient (ad hoc)
Failure rates (first year)
Perfect useSymptoms-based: 1-3%
Calendar-based: 5-9%
Typical use3-25%
Usage
ReversibilityYes
User remindersDependent upon strict user adherence to methodology
Clinic reviewNone
Advantages and disadvantages
STD protectionNo
PeriodsIncreased prediction
Benefitsno side effects, can aid pregnancy achievement

Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba , (FA) unarejelea jumla ya mambo yanayotumiwa kuamua wakati mwanamke anapoweza kushika mimba na asipoweza kushika mimba katika mzunguko wa hedhi. Mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba zinaweza kutumiwa ili kuzuia mimba, na kutunga mimba, au kama njia ya kusimamia afya ya uzazi wa mwanamke.

Mbinu za kubaini siku ambazo mwanamke hawezi kupata mimba zinajulikana tangu zamani, lakini ujuzi wa kisayansi uliopatikana katika karne ya iliyopita imeongezeka sana usahihi wa mbinu hizo. Kutoka 1930-1980, utafiti wote na ukuzaji wa uelewa wa masuala ya uzazi ulifanywa na wanaohusishwa na Kanisa Katoliki la Kirumi. Mashirika ya ufahamu wa uwezo wa kushika mimba yanaendelea kudhibitiwa na Katoliki, lakini baadhi ya mashirika ya kawaida sasa yapo.

Mifumo ya ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hutegemea uchunguzi wa mabadiliko ya ishara moja au zaidi ya kimsingi yanayoashiria uwezekano wa kutunga mimba (joto la kimsingi la mwili, kamasi ya seviksi, na mkao wa seviksi), kufuatilia mzunguko wote wa hedhi na kubaini wakati ambapo inawezekana kushika mimba kulingana na habari hii, au zote mbili. Ishara nyingine pia zinaweza kuzingatiwa: hizi ni pamoja na ulaini wa matiti na miteliskimazi (uchungu wakati yai linapoachiliowa), uchunguzi wa vifaa vya kukagua mkojo vinavyojulikana kama vifaa vya kubashiri mayai, ufupisho Kiingereza (OPKs), na uchunguzi wa kihadubini wa mate au ugiligili wa seviksi. Pia njia ya kufuatilia uwezo wa kushika mimba kwa tarakilishi unapatikana.

Istilahi

Mbinu zinazotegemea dalili zinahusisha kufuatilia ishara moja au zaidi kati ya ishara tatu za kimsingi za kuweza kutunga mimba - joto la kimsingi la mwili, kamasi ya seviksi, na mkao wa seviksi.[1] Mifumo zinazotegemea kamasi ya seviksi ni pamoja na Mtindo wa Billing wa Kutambua Yai, Mtindo wa Creighton, na Mbinu ya Siku Mbili. Mbinu za dalili za joto la mwili hujumuisha uchunguzi wa joto la kimsingi la mwili (BBT), kamasi ya seviksi, na wakati mwingine mkao wa seviksi. Mbinu za kalenda hutegemea kufuatilia mzunguko wa hedhi ya mwanamke na urefu wa mzunguko wake kutambua anapoweza kutunga mimba. Mbinu bora inayojulikana kati ya hizi ni Mbinu ya Siku Wastani ambayo ndiyo msingi wa mbinu ya kutazamwa kutumia kifaa kiitwacho CycleBeads. Mbinu ya Urari-Kalenda pia huzingatiwa njia ya kutegemea kalenda, ingawa haijafanuliwa vizuri na ina maana tofauti kwa watu tofauti.

Mifumo za ufahamu wa uzazi zinaweza kutatwa kuwa Mbinu za Uzazi zinazoegemea Ufahamu(mbinu za MUUFA ), [2] istilahi Mbinu za Uelewa wa Uzazi (MUU) inahusu hasa mfumo uliofundisha na Toni Weschler. Neno "mbinu asili ya uzazi wa mpango" (NFP) wakati mwingine hutumiwa kutaja matumizi ya mbinu yoyote ya Ufahamu wa Uzazi FA. Hata hivyo, NFP kimahsusi inahusu mbinu zilizoidhinishwa na Kanisa Katoliki: kutoweza kutungisha wakati wa kunyonyesha, na kutoshiriki ngono katika kipindi ambapo kuna uwezekano wa kupata mimba. Mbinu ya FA inaweza kutumika kwa watumiaji NFP kutambua nyakati hizi rutuba.

Wanawake wanaonyonyesha na wangependelea kuzuia mimba wanaweza kutumia mbinu ya kukatizwa kwa hedhi wakati wa kunyonyesha (LAM). LAM ni tofauti na ufahamu wa uzazi, lakini kwa sababu haihusishi vifaa au kemikali, mara nyingi huwasilishwa pamoja na Ufahamu wa Uzazi FA kama njia ya kudhibiti uzazi.

Historia

Ukuaji wa mbinu zinazotegemea kalenda

Haijulikani hasa ni wakati gani iligunduiwa kwa mara ya kwanza kuwa wanawake wana vipindi vya kutunga mimba na visivyo vya kutunga mimba vinavyoweza kutabirika. Mt. Agustino aliandika kuhusu uepukaji ngono ili kuzuia mimba katika mwaka wa 388 ( Wamanicheani walijaribu kutumia njia hii ili kubakia bila watoto, na Agustino akashutumu matumizi yao ya kuacha kushiriki ngono kwa kipindi fulani).[3] Kitabu kimoja kinasema kwamba kuacha kushiriki ngono kwa muda kulipendekezwa na " watu wachache wasio wa kidini tangu katikati ya karne ya kumi na tisa," [4] lakini ushawishi mkuu katika karne ya ishirini uliohamasisha mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ulitoka katika Kanisa Katoliki.

Mnamo 1905 Theodoor Hendrik van de Velde, mwanajinakolojia wa Kiholanzi, alionyesha kuwa wanawake hutoa yai mara moja tu katika mzunguko wa hedhi.[5] Mnamo 1920, Kyusaku Ogino, mwanajinakolojia wa Kijapani, na Hermann Knaus, kutoka Austria, wakifanya kazi mbalimbali waligundua kwamba yai hutokea yapata siku kumi na nne kabla ya kipindi cha hedhi inayofuata.[6] Ogino alitumia ugunduzi wake kutengeneza mfumo wa kutumiwa katika kuwasaidia wanawake kupata mimba kwa muda wa ngono na kufikia mimba. Mnamo 1930, John Smulders, daktari wa Mkatoliki kutoka Uholanzi, alitumia ugunduzi huu kuunda mbinu ya kuepuka mimba. Smulders alichapisha kazi yake kwa chama cha matabibu wa Kikatoliki cha Uholanzi, na huu ulikuwa mfumo wa kwanza rasmi wa kuacha kujamiiana kwa kipindi fulani - mbinu ya urari.[6]

Uanzilishi wa mbinu za dalili za joto na kamasi ya mlango wa uzazi

Katika miaka ya 1930, Rev. Wilhelm Hillebrand, padri wa Kikatoliki nchini Ujerumani, alibuni mfumo wa kuzuia mimba kutegemea joto la kimsingi la mwili.[7] Mbinu hii ya joto ilipatikana kuwa na ufanisi zaidi katika kuwasaidia wanawake kuzuia mimba kuliko mbinu ya kutegemea kalenda. Katika miongo michache iliyofuata, mifumo hii miwili ikawa inatumika sana miongoni mwa wanawake Wakatoliki. Hotuba mbili zilizotolewa na Papa Pius XII mnamo 1951 zilitoa kielelezo cha juu cha kutambuliwa kwa mbiu hizi na Kanisa Katoliki-kwa mume na mke waliotaka kuzuia mimba.[4][8] Katika mwanzo wa miaka ya 1950, Dkt. John Billings aligundua uhusiano kati ya kamasi ya mlango wa uzazi na uwezekano wa kutunga mimba alipokuwa akiifanyia kazi katika Shirika la Kikatoliki la Usatawi wa Kijamii mjini Melbourne. Dkt. Billings na madaktari wengine kadhaa walitafiti ishara hii kwa miaka kadhaa, na kufikia mwishoni mwa miaka ya 1960 walikuwa wakifanya majaribio ya kkimatibabu na kuanzisha vituo vya kufundisha duniani kote.[9]

Mashirika ya kwanza ya ufundishaji yaliyozingatia dalili

Japo awali Dkt. Billings alifundisha dalili za joto na kamasi, walipata tatizo katika kufundisha ishara za joto kwa idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika katika nchi zinazoendelea. Katika miaka ya 1970 walibadilisha mbinu hiyo ili kutegemea kamasi tu.[7] Jumuiya ya kimataifa iliyoanzishwa na Dkt. Billings sasa inajulikana kama Shirika la Watumiaji Mbinu ya Billings Duniani (WOOMB).

Shirika la kwanza kufundisha mbinu za dalili na joto lilianzishwa mwaka 1971. John na Sheila Kippley, waumini wa kawaida Wakatoliki, walijiunga na Dkt. Konald Prem katika kufundisha mbinu ya kutazama iliyotegemea dalili zote tatu: joto, kamasi, na pia mkao wa mlango wa uzazi. Shirika lao sasa linaitwa Shirika la Wanandoa kwa Wanandoa la Kimataifa (Couple to Couple League International).[7] Muongo uliofuata ulishuhudia kuanzishwa kwa mashirika mengine ya Kikatolikiambayo sasa ni makubwa - Family of the Americans (1977), mafundisho ya mbinu za Billings,[10] na Taasisi ya Papa Paulo VI (1985), inayofundisha mbinu ya kamasi pekee iitwayo Creighton Model.[11]

Hadi miaka ya 1980, habari kuhusu ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ulipatikana tu kutoka katika vyanzo vya Kikatoliki.[12] Shirika la kwanza lisilo la kidini la mafundisho ya uzazi lilikuwa Kituo cha Uelewa wa Uzazi cha New York, lililoanzishwa mwaka 1981.[13] Toni Weschler alianza kufundisha manamo 1982 na kuchapishwa kitabu kilichouza sana cha Taking Charge of Your Fertility katika mwaka wa 1995.[14] Justisse ilianzishwa mwaka 1987 Edmonton, Kanada.[15] Mashirika haya yote yasiyo ya kidini yanafundisha mbinu za dalili na joto. Ingawa mashirika ya kikatoliki ni makubwa sana kuliko mashirika ya kiharakati yasiyo ya kidni yanayoshughulikia uzazi, walimu wasiyo wa kujitegemea wa kidini wameongezeka zaidi katika miaka ya 1990 na 2000.

Ustawishaji unaoendelea

Ustawi wa mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaoendelea. Mwishoni mwa miaka ya 1990, Taasisi ya Afya ya Uzazi katika Chuo Kikuu cha Georgetown ilianzisha mbinu mbili mpya.[16][17] Mbinu ya Siku Mbili, Mfumo wa kamasi tu, na CycleBeads, ni kibadala cha mbinu ya Mbinu ya Urari, zimeundwa ili kuwa na ufanisi mkubwa na rahisi katika kufundisha, kujifunza, na matumizi.

Ishara za uwezo wa kushika mimba

Mizunguko nyingi ya hedhi huwa na siku kadhaa za mwanzo ambapo mimba haiwezi kushika (muda wa kutoshika mimba kabla ya kudondosha yai), siku ambazo mimba inaweza kutungika, na kisha siku kadhaa tu kabla ya hedhi ambazo mimba haiwezi kutungika ( muda wa kutoshika mimba wa baada ya yai kudondoshwa). Siku ya kwanza ya kuvuja damu nyekundu inahesabiwa kuwa siku ya kwanza ya mzunguko wa hedhi. Mifumo mbalimbali ya ufahamu wa uwezo wa kushika mimba huhesabu kipindi ambapo kuna uwezekano wa kupata mimba kwa njia tofauti kidogo, kutumia ishara za kimsingi za uwezekano wa kutunga mimba, historia ya mzunguko, au zote mbili.

Ishara za msingi

Ishara tatu za msingi za uwezekano wa kushika mimba ni joto msingi la mwili (BBT), kamasi ya seviksi, na mkao wa seviksi. Mwanamke anayetumia dalili msingi za uwezo wa kutunga mimba anaweza kuchagua kutumia ishara moja, ishara mbili, au, zote tatu.

Joto la msingi la mwili ni joto la mwili wa mtu wa linalochukuliwa wakati wa kwanza anapoamka asubuhi (au baada ya usingizi wao wa muda mrefu wa siku). Miongoni mwa wanawake, kudondoshwa yai husababisha kupanda kwa BBT kwa kati ya 0.3 na 0.9 ° C (0.5 na 1.6 ° F) ambayo hubakia hivyo katika kipindi chote hadi wakati wa hedhi ijayo. Mabadiliko haya ya joto yanaweza kutumika kubaini mwanzo wa kipindi cha kutotunga kabla ya kudodosha yai.

Kamasi ya seviksi

Kuonekana kwa kamasi ya seviksi na mwasho wa uke ni ishara zinazoelezwa kwa pamoja kama njia mbili za kubaini ishara hiyo. Kamasi ya seviksi huzalishwa na seviksi, ambayo hutenganisha uterasi na mfereji wa uke. Kamasi ya seviksi yenye uwezo wa kushika mimba hukuza maisha ya manii kwa kupunguza uasidi wa uke, na pia husaidia kuongoza manii kupitia seviksi kuelekea ndani ya uterasi. Uzalishaji wa kamasi ya seviksi yenye rutuba husababishwa na homoni moja (istrojeni) ambayo pia huandaa mwili wa mwanamke kwa udondoshwaji wa yai. Kwa kuangalia kamasi yake ya seviksi, na kuzingatia hisia ya jinsi inavyopita ukeni, mwanamke anaweza kubaini wakati mwili wake unapojiandaa kudondosha yai, na pia wakati ambapo udondoshwaji wa yai umepita. Wakati yai limedondoshwa, uzalishwaji wa istrojeni hupungua na projesteroni huanza kuongezeka. Kupanda kwa kiwango cha projesteroni husababisha mabadiliko katika wingi na hali ya kamasi inayopatikana katika uke.[18]

Seviksi hubadilisha mkao kutokana na homoni sawa inayosababisha kutolewa kwa kamasi ya seviksi kukauka. Wakati mwanamke yuko katika awamu ya kutoshika mimba ya mzunguko wa hedhi, seviksi hushuka chini katika mfereji wa uke, ikiguswa huwa ngumu (kama ncha ya pua ya mtu), na, upenyu - kipenyo kinachoelekea katika seviksi - itakuwa kidogo ikilinganishwa na wakati mwingine, au 'funge'. Jinsi mwanamke anavyoongezeka kuwa na uwezo wa kushika mimba ndivyo seviksi kinavyopanda juu ya mfereji wa uke, ni laini ukiguswa (laini kama mdomo wa mtu), na upenyu utakuwa wazi zaidi. Baada ya kudondoshwa kwa yai, seviksi itarejea katika mkao wake wa wakati ambapo si wa kushika mimba.

Historia ya mzunguko

Mifumo inayotegemea kalenda hubainisha uwezekano wa kutopata mimba wa kabla na baada ya kudondosha yai kulingana na historia ya mzunguko. Yanapotumia kuzuia mimba, mifumo hii ina umadhubuti wa juu ukilinganishwa na mifumo inayotegemea dalili, hata hivyo umadhubuti wake ni wa chini ukilinganishwa na mbinu zuizi kama vile kiwambo na vizibo vya seviksi

Mbinu zinazotegemea kamasi na joto la mwili kubaini uwezo wa kutunga mimba zinapotumiwa kuepuka mimba, hudhihirisha matokeo katika matumizi ya chini sana mimba viwango-kamilifu.[19] Hata hivyo, mifumo ya kamasi na joto la mwili huwa na upungufu fulani katika kubaini uwezo wa kutotunga mimba kabla ya kudondosha yai. Rekodi ya joto la mwili pekee haitoi mwongozo wa uwezekano wa kutunga au kutotunga mimba kabla ya yai kudondoshwa. Kubaini uwezekano wa kutoshika mimba kunaweza kufanywa kwa kuchunguza kamasi ya seviksi; hata hivyo, hii hushuhudia matokeo yenye kiwango cha chini cha ufanisi zaidi kuliko ile inayoshuhudiwa katika kipindi cha uwezo wa kutokutungisha baada ya kudondosha yai.[20] Kutegemea uchunguzi wa kamasi pekee pia ina maana kwamba kufanya ngono bila kinga hairuhusiwi wakati wa hedhi, kwa sababu kamasi yoyote haitakuwa dhahiri.[21]

Matumizi ya sheria fulani za kalenda kuamua urefu wa kipindi cha kutoweza kutunga mimba kabla ya yai kudondoshwa huruhusu siku chache za ngono zembe katika siku za kwanza za mzunguko wa hedhi huku kukiwa na kiwango cha chini sana cha uwezekano wa kupata mimba.[22] Kwa kutumia mbinu ya kamasi pekee, kuna uwezekano wa kutambua kimakosa kipindi cha katikati ya mzunguko wa hedhi au kutoka damu katika mzunguko wa hedhi ambapo yai halikudondoshwa. Kuweka chati sahihi ya Joto la Kimsingi la Mwili huwezesha utambuzi sahihi wa hedhi, wakati ambapo sheria za kalenda zinazoshughulika na kipindi kabla ya kudondosha yai zinaweza kutumiwa.[23] Katika mifumo ya joto pekee, sheria ya kalenda inaweza kutegemewa pekee kuamua uwezekano wa kutoshika mimba kabla ya kudondosha yai. Katika mifumo ya joto na ishara, sheria ya kalenda huthibitishwa kwa rekodi za kamasi: uchunguzi wa kamasi ya seviksi unaoashiria uwezo wa kupata mimba unapewa kipaumbele kuliko mbinu yoyote ya kalenda ya kubainisha uwezo wa kushika mimba.[22]

Sheria za kalenda zinaweza kuweka idadi mahsusi ya siku, inayobainisha kwamba (kulingana na urefu wa mizunguzo iliyopita ya hedhi) siku tatu hadi sita za kwanza katika kila mzunguko wa hedhi huchukuliwa kuwa isiyo na uwezo wa kupata mimba.[24] Au, sheria ya kalenda inaweza kuhitaji hesabu, kwa mfano lazima iwe kwamba urefu wa kipindi kabla ya kudondosha yai ni sawa na urefu wa muda mfupi zaidi sana wa mzunguko wa hedhi ukiondoa siku ishirini na moja.[25] Badala ya kufungiwa katika urefu wa mzunguko, sheria ya kalenda inaweza kubuniwa kutokana na siku ya mzunguko ambapo mwanamke ameshuhudia mabadiliko katika joto la mwili. Mfumo mmoja unasema urefu wa kipindi cha kutoweza kutunga mimba kabla ya kudondosha yai unalingana na siku ya kwanza ambapo mwanamke aliposhuhudia kupanda joto la mwili ondoa siku saba.[26]

Ishara andamizi

Wanawake wengi huhisi ishara andamizi za uzazi zinazohusiana na awamu fulani ya mzunguko wa hedhi. Mifano ni pamoja na maumivu ya tumbo na uzito, maumivu ya mgongo, ulaini wa matiti na miteliskmazi (maumivu ya kudondosha yai).

Mbinu nyinginezo

Vifaa vya kubashiri udondoshwaji wa yai (OPKs) inaweza kuchunguza udondoshwaji unaotarajiwa kutegemea wingi wa homoni ya kuandaa ukuta wa chupa ya kizazi, ufupisho wa Kiingereza (LH) katika mkojo na mwanamke. Ubashiri wa undondoshaji wa kufana, hufuatiwa na udondoshaji ndani ya saa 12-36.

Uchunguzi hadubini wa mate, ukifanyika kwa usahihi, unaweza kugundua vijidutu maalum katika mate ambavyo hutangulia udondoshwaji wa yai. Vijidutu hivyo kwa kawaida huonekana siku tatu kabla ya udondoshwaji yai, na kuendelea mpaka udondoshaji utokee. Katika kipindi hiki, vijidutu hivi hutokea katika kamasi ya seviksi pamoja na mate.

Vichunguza uzazi vinapatikana kwa majina mbalimbali ta kibiashara. Vichunguzi hivi vinaweza kutumia mifumo Joto la Kimsingi la Mwili BBT pekee, vinaweza kuchanganua vitepe vya kupima mkojo, au vinaweza kuchunguza ukinzani meme wa mate na ugiligili wa uke.

Faida na upungufu

Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba una kiwango fulani cha sifa bainifu:

  • Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumika kudhibiti afya ya uzazi. Mabadiliko katika mzunguko wa hedhi yanaweza kumtahadharisha mtumiaji kuhusu kujitokeza kwa matatizo ya kiginakolojia. Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba pia unaweza kutumika kusaidia katika kuagua matatizo yanayojulikana ya kijinakolojia kama vile kutoweza kushika mimba.
  • Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ni uwanda mpana: unaweza kutumika kuzuia mimba au kusaidia katika kutunga mimba.
  • Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumiwa na wanawake wote katika kipindi chote cha uzazi, bila kujali ikiwa anakaribia kumaliza kuzaa, ananyonyesha, au anapata mzunguko wa hedhi usio wa kawaida kwa sababu zingine.
  • Matumizi ya ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutoa ufahamu kuhusu jinsi mwili wa mwanamke unavyofanya kazi, na unaweza kuwaruhusu wanawake kuwa na udhibiti mkubwa wa uzazi wao wenyewe.
  • Aina fulani ya mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba zinazotegemea dalili ya uzazi zinahitaji uchunguzi au kugusa kamasi ya seviksi, matendo ambayo baadhi ya wanawake hawafurahii. Baadhi ya wahudumu wanapendelea kutumia neno "majimaji ya seviksi" badala ya kamasi ya seviksi, katika juhudi ya kuwafanya wanawake kama hao kuhisi huru kidogo.
  • Baadhi ya dawa, kama vile ya kupunguza kupaliwa mapafuni, yanaweza kubadili kamasi ya kizazi. Kwa wanawake wanaotumia dawa hizi, ishara ya kamasi huenda isionyeshe kisahihi uwezo wa kutunga mimba .[27]
  • Baadhi ya mbinu zinazotegemea dalili huhitaji ufuatiliaji wa joto la kimsingi ya mwili. Kwa sababu usingizi usiokuwa na utaratibu unaweza kuvuruga usahihi wa joto la kimsingi la mwili, wafanyakazi wa kubadilisha zamu na walio na watoto wadogo sana, kwa mfano, huenda wasiweze kutumia mbinu hizo.[27]

Kama njia ya kupanga uzazi

Kwa kuhakikisha kuwa ngono bila kinga inafanyika katika sehemu ambapo mimba haiwezi kushikika katika mzunguko wa hedhi, mwanamke na mpenzi wake wanaweza kuzuia mimba. Wakati ambapo mimba inaweza kushikwa katika mzunguko wa hedhi, wanandoa wanaweza kutumia mbinu za kukinga mimba au waache kushiriki ngono.

Manufaa

  • Hakuna madhara yanayohusishwa na dawa katika ufahamu wa uwezo wa kushika mimba. Hakuna madhara yoyote ya utumiaji, isipokuwa azinazoweza kutokea kwa kuingiza vidole ndani ya uke ili kuchunguza seviksi (kama inavyopendekezwa na baadhi ya mbinu ufahamu wa uwezo wa kushika mimba).
  • Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hauna malipo au gharama ni nafuu sana. Watumiaji wanaweza kununua chati, kalenda, kipima joto cha msingi, au mifumo ya tarakilishi, au kumwajiri mkufunzi. Gharama ya moja kwa moja ni ya chini ikilinganishwa na mbinu nyingine.
  • Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumika pamoja na vifaa vya kuzuia mimba ili kujamiiana kuendelea katika kipindi chote ambapo kuna uwezekano wa kupata mimba. Tofauti na utumiaji wa vifaa vya kuzuia mimba bila kutumia Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba, utumiaji wa ufahamu wa uwezo wa kushika mimba kunaweza kuwaruhusu wapenzi kutumia vizuia mimba wakati ambapo ni muhimu tu.

Mapungufu

  • Matumizi ya zana za kizuia mimba yanahitajika katika kipindi ambapo mimba inaweza kutungwa, la sivyo lazima wanandoa waachae kushiriki ngono. Kupunguza mimba uwezekano wa kupata mimba kuwa chini ya 1% kila mwaka, kuna takriban siku 13 ambapo kushiriki ngono au vizuizi lazima vitumika wakati wa kila mzunguko mmoja.[28] Kwa wanawake wasio na mzunguko inayo badilika badilika sana - kama ilivyo kawaida wakati wa kunyonyesha, baada ya kufunga uzazi, au kama ilivyo kwa walio na magonjwa ya homoni kama vile PCOS - kuacha kujamiiana au matumizi ya vizuizi kunaweza kuhitajika katika miezi fulani. Wapenzi wengi huenda wasiwe na motisha au nidhamu ya kuacha kujamiiana au kutumia vizuizi kwa muda mrefu.
  • Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hauzuii dhidi ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa.[29]

Ufaafu

Ubora wa ufahamu ya uzazi, kama ulivyo na mbinu nyingi za kuzuia mimba, inaweza kutathmini kwa njia mbili. Viwango vya utumizi kamili au vya ubora wa mbinu huzingatiwa kwa watu wanaofuata sheria zote pekee, tambua kwa usahihi kipindi ambapo kuna uwezekano wa kutunga mimba, na uache kushiriki ngono bila kinga katika siku ulizotambua kuwa kuna uwezekano wa kutunga mimba. Viwango vya ubora vya matumizi halisi, au matumizi ya kawaida ni kwa wanawake wote wanaotegemea ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ili kuzuia mimba, ikiwa ni pamoja na wasioweza kutimiza vigezo vya "matumizi kamili". Viwango kwa kawaida huwasilishwa katika mwaka wa kwanza wa matumizi.[30] Kwa kawaida mfumo wa Pearl Index hutumika kukokotoa viwango vya ubora, lakini baadhi ya tafiti hutumia majedwali ya mapunguzo.[31]

Kiwango cha kufeli kwa ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hutofautiana pakubwa kulingana na mfumo uliotumika kubaini uwezekano wa kupata mimba, njia ya mafundisho, na idadi ya wanaotafitiwa. Baadhi ya tafiti zimepata viwango halisi vya kufeli vya 25% kwa mwaka au zaidi.[32][33][34] Angalau utafiti mmoja umepata kiwango cha kufeli cha chini ya 1% kwa mwaka kukiwa na mafundisho endelevu na mapitio ya kila mwezi,[35] na tafiti kadhaa zimegundua viwango vya kufeli halisi vya 2-3% kwa mwaka.[36][37][28][38]

Inapotumika kwa usahihi, na kuandamana na mafundisho endelevu ya mara kwa mara, baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa aina fulani za Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba huwa na 99% ufanisi,[39][40][35][41] ulio sawa na wa tembe za kuzuia mimba.[42]

Kutoka katika Teknolojia ya Uzazi: [43]

  • Mbinu za baada ya kudondosha yai (yaani kuacha kushiriki ngono kutoka wakati wa hedhi mpaka baada ya kudondoshwa) ina kiwango cha kufeli cha 1% kwa mwaka.
  • Mbinu ya dalili na joto la mwili ina kiwango cha kufeli cha 2% kwa mwaka.
  • Mbinu ya kamasi ya mlango wa kisasi pekee ina kufeli kwa kiasi cha 3% kwa mwaka.
  • Mbinu ya urari wa kalenda una kiwango cha kufeli kwa 9% kwa mwaka.
  • Mbinu ya Siku Wastani una kiwango cha kufeli kwa 5% kwa mwaka.

Sababu za ufanisi mdogo katika utumizi wa kawaida

Sababu kadhaa zinachangia ufanisi wa matumizi ya kawaida kuwa ya chini zaidi kuliko ufanisi katika matumizi kamili:

  • makosa kwa upande wa watoa maelezo ya jinsi ya kutumia mbinu hii (mkufunzi kutoa taarifa isiyo sahihi au isiyokamili kuhusu mfumo wa sheria)
  • makosa kwa upande wa mtumiaji (kutoelewa sheria, makosa katika kunakili)
  • kutotii maelezo kimakusudi kwa watumiaji (kushiriki ngono zembe katika siku ambapo mimba inaweza kutungwa)

Sababu ya kawaida kwa ufanisi halisi wa chini si makosa kwa upande wa wakufunnzi au watumiaji, bali kutokana na mtumiaji kutotii sheria kimakusudi,[28][41], yaani wanandoa kujua kwamba mwanamke anaweza kutunga mimba wakati huo, lakini wakajihusisha katika ngono zembe bila kujali. Hii ni sawa na kufeli kwa mbinu zuizi, ambazo kimsingi husababishwa na kutotumia mbinu hizo.

Ili kupata mimba

Kupima wakati wa kujamiiana

Utafiti uliofanywa na Barrett na Marshall umeonyesha kuwa vitendo vya ngono visivyopangiwa huwa na uwezekano wa 24% kutungisha mimba katika mzunguko wa hedhi. Utafiti huo pia uligundua kuwa ngono inayolenga wakati maalumu kulingana na ufahamu unaotokana na mbinu ya joto la kimsingi la mwili pekee ambayo ni mbinu ya Ufahamu wa Uzazi huongeza viwango vya mimba kwa 31% -68%.

Utafiti wa mbinu ya kamasi ya seviksi umegundua viwango vya mimba vya 67% -81% katika mzunguko wa kwanza ikiwa kujamiiana kutatokea katika Siku ya Kilele cha ishara za kamasi.[44][45]

Kwa sababu ya viwango vya juu vya kutoka mimba mapema (25% ya mimba hupotea katika wiki sita za kwanza tangu hedhi ya mwisho iliyopita ya mwanamke, au LMP), mbinu inayotumika kuchunguza mimba inaweza kusababisha upendeleo katika viwango vya mimba. Mbinu zilizo na uwezo wa kuonyesha mabadiliko madogo zaidi zinaweza kuonyesha viwango vya chini vya utungaji mimba, kwa sababu huwa zinakosa matokeo yaliyosababisha mimba kutoka mapema. Utafiti mmoja nchini Uchina kati ya wapenzi wanaoshiriki ngono bila mpangilio ili kutungisha mimba ulitumia mbinu ya kupima za kuchunguza mabadiliko madogo zaidi kugundua mimba. Ilipata kiwango cha 40% cha kutungwa mimba kwa kila mzunguko katika kipindi cha utafiti wa miezi 12.[46]

Uaguzi wa matatizo

Mizunguko ya kawaida ya hedhi wakati mwingine huchukuliwa kuwa ushahidi kwamba mwanamke anadondosha mayai kawaida, na mizunguko isiyo ya kawaida kuwa ushahidi kuwa udondoshaji wa yai si wa kawaida.[47] Hata hivyo, wanawake wengi walio na mizunguko isiyo ya kawaida hudondosha mayai kwa kawaida, na baadhi walio na mizunguko ya kawaida kwa kweli hawadondoshi mayai au wana matatizo katika awamu ya kutayarisha ukuta wa chupa cha uzazi. Rekodi za joto la kimsingi la mwili, hasa, lakini pia rekodi za kamasi ya seviksi na mkao wake, inaweza kutumika kwa usahihi kung'amua ikiwa mwanamke ana dondosha yai, na kama urefu wa kipindi cha baada ya kudondosha yai cha mzunguko wa hedhi inatosha kuendeleza ujauzito.

Kamasi ya seviksi unaoweza kutunga mimba ni muhimu katika kujenga mazingira ambayo yanaruhusu manii kupita katika mlango wa uzazi na katika viriba falopu ambako husubiri kudondoshwa kwa yai.[48] Chati za uzazi zinaweza kusaidia kuagua kamasi hasimu kwa uwezo wa mimba kutungishwa, sababu ya kawaida ya kutokutungisha mimba. Ikiwa hali hii itaaguliwa, baadhi ya washauri wanapendekeza matumizi ya guaifenesini katika siku chache kabla ya udondoshwaji wa yai ili kupunguza uzito wa kamasi.[49]

Upiamji mimba na umri wa ujauzito

Vipimo vya mimba si sahihi mpaka baada ya wiki 1-2 baada ya kudondoshwa yai. Kujua tarehe inayokisiwa yai itadondoka kunaweza kumzuia mwanamke kupata matokeo yasiyo sahihi kutokana na upimaji wa mapema mno. Pia, siku 18 mfululizo ya joto iliyopanda, ina maanisha mwanamke ni mjamzito bila shaka.[50]

Makadirio ya tarehe ya kudondosha yai kutoka katika chati za uzazi ni njia sahihi zaidi ya kukadiria umri wa ujauzito zaidi ya mbinu za jadi za kupima mimba au mbinu ya kuchunguza hedhi ya mwisho katika utaratibu wa kufuatilia hedhi.[51]

Marejeleo zaidi

  • Toni Weschler (2006). Taking Charge of Your Fertility (toleo la 10th Anniversary). New York: Collins. ISBN 0-06-088190-9.
  • John F. Kippley and Sheila K. Kippley (1996). The Art of Natural Family Planning (toleo la Fourth). Cincinnati, OH: Couple to Couple League International. ISBN 0-926412-13-2.

Tanbihi

  1. Weschler, Toni (2002). Taking Charge of Your Fertility (toleo la Revised). New York: HarperCollins. uk. 52. ISBN 0-06-093764-5.
  2. "Medical Eligibility Criteria for Contraceptive Use:Fertility awareness-based methods". Third edition. World Health Organization. 2004. Iliwekwa mnamo 2007-06-12. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)
  3. Saint, Bishop of Hippo Augustine (1887). A Select Library of the Nicene and Post-Nicene Fathers of the Christian Church, Volume IV. Grand Rapids, MI: WM. B. Eerdmans Publishing Co. ku. On the Morals of the Manichæans, Chapter 18. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  4. 4.0 4.1 Yalom, Marilyn (2001). A History of the Wife (toleo la First). New York: HarperCollins. ku. 297–8, 307. ISBN 0-06-019338-7.
  5. "A Brief History of Fertility Charting". FertilityFriend.com. Iliwekwa mnamo 2006-06-18.
  6. 6.0 6.1 Singer, Katie (2004). The Garden of Fertility. New York: Avery, a member of Penguin Group (USA). ku. 226–7. ISBN 1-58333-182-4.
  7. 7.0 7.1 7.2 Hays, Charlotte (2001). "Solving the Puzzle of Natural Family Planning". Crisis Magazine. Iliwekwa mnamo 2007-03-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  8. [18] ^ Moral Questions Affecting Married Life: Addresses given October 29, 1951 to the Italian Catholic Union of midwives November 26, 1951 to the National Congress of the Family Front and the Association of Large Families, National Catholic Welfare Conference, Washington, DC.
  9. Billings, John (2002). "THE QUEST — leading to the discovery of the Billings Ovulation Method". Bulletin of Ovulation Method Research and Reference Centre of Australia. 29 (1): 18–28. Iliwekwa mnamo 2007-03-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  10. "About us". Family of the Americas. 2006. Iliwekwa mnamo 2007-03-18.
  11. "About the Institute". Pope Paul VI Institute. 2006. Iliwekwa mnamo 2007-03-18.
  12. Singer (2004), p.xxiii
  13. "About us". Fertility Awareness Center. 2006. Iliwekwa mnamo 2007-03-18.
  14. Weschler (2002)
  15. "About Us". Justisse. 2002. Iliwekwa mnamo 2007-03-18.
  16. Arévalo M, Jennings V, Sinai I (2002). "Efficacy of a new method of family planning: the Standard Days Method" (PDF). Contraception. 65 (5): 333–8. doi:10.1016/S0010-7824(02)00288-3. PMID 12057784.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  17. Jennings V, Sinai I (2001). "Further analysis of the theoretical effectiveness of the TwoDay method of family planning". Contraception. 64 (3): 149–53. doi:10.1016/S0010-7824(01)00251-7. PMID 11704093.
  18. James B. Brown (2005). "Physiology of Ovulation". Ovarian Activity and Fertility and the Billings Ovulation Method. Ovulation Method Research and Reference Centre of Australia.
  19. [39] ^ Kippley (2003), uk.121-134 ,376-381
  20. [40] ^ Kippley (2003), uk.114
  21. Evelyn, Dr. Billings, Ann Westinore, (1998). The Billings Method: Controlling Fertility Without Drugs or Devices. Toronto: Life Cycle Books. uk. 47. ISBN 0-919225-17-9.{{cite book}}: CS1 maint: extra punctuation (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  22. 22.0 22.1 [43] ^ Kippley (2003), uk.108-113
  23. [44] ^ Kippley (2003), uk.101 sidebar na Weschler (2002), uk.125
  24. [46] ^ Kippley (2003), uk.108-109 na Weschler (2002), uk.125-126
  25. [47] ^ Kippley (2003), uk.110-111
  26. [48] ^ Kippley (2003), uk.112-113
  27. 27.0 27.1 "How to Observe and Record Your Fertility Signs". Fertility Friend Handbook. Tamtris Web Services. 2004. Iliwekwa mnamo 2005-06-15.
  28. 28.0 28.1 28.2 Frank-Herrmann P, Heil J, Gnoth C; na wenz. (2007). "The effectiveness of a fertility awareness based method to avoid pregnancy in relation to a couple's sexual behaviour during the fertile time: a prospective longitudinal study". Hum. Reprod. 22 (5): 1310–9. doi:10.1093/humrep/dem003. PMID 17314078. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  29. "Natural family planning". University of Iowa Health Care Website. McKesson Health Solutions. 2003. Iliwekwa mnamo 2006-06-15.
  30. Hatcher, RA (2000). Contraceptive Technology (toleo la 18th). New York: Ardent Media. ISBN 0-9664902-6-6. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  31. Kippley, John (1996). The Art of Natural Family Planning (toleo la 4th addition). Cincinnati, OH: The Couple to Couple League. uk. 141. ISBN 0-926412-13-2. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  32. Wade ME, McCarthy P, Braunstein GD; na wenz. (1981). "A randomized prospective study of the use-effectiveness of two methods of natural family planning". American journal of obstetrics and gynecology. 141 (4): 368–376. PMID 7025639. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  33. Medina JE, Cifuentes A, Abernathy JR; na wenz. (1980). "Comparative evaluation of two methods of natural family planning in Colombia". American journal of obstetrics and gynecology. 138 (8): 1142–1147. PMID 7446621. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  34. Marshall J (1976). "Cervical-mucus and basal body-temperature method of regulating births: field trial". Lancet. 2 (7980): 282–283. doi:10.1016/S0140-6736(76)90732-7. PMID 59854. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  35. 35.0 35.1 [76] ^ Evaluation of the Effectiveness of a Natural Fertility Regulation Programme in China : Shao-Zhen Qian, et al. Reproduction and Contraception (English edition), in press 2000.
  36. Frank-Herrmann P, Freundl G, Baur S; na wenz. (1991). "Effectiveness and acceptability of the sympto-thermal method of natural family planning in Germany". American journal of obstetrics and gynecology. 165 (6 Pt 2): 2052–2054. PMID 1755469. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  37. Clubb EM, Pyper CM, Knight J (1991). "A pilot study on teaching natural family planning (NFP) in general practice". Proceedings of the Conference at Georgetown University, Washington, DC. http://www.fertilityuk.org/nfps822.html.
  38. Frank-Herrmann P, Freundl G, Gnoth C; na wenz. (Juni–Septemba 1997). "Natural family planning with and without barrier method use in the fertile phase: efficacy in relation to sexual behavior: a German prospective long-term study". Advances in Contraception. 13 (2–3): 179–189. doi:10.1023/A:1006551921219. PMID 9288336. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: date format (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  39. Ecochard, R.; Pinguet, F., Ecochard, I., De Gouvello, R., Guy, M., na Huy, F. (1998) "Analysis of natural family planning failures. Katika 7007 mzunguko wa kutumia ", In 7007 cycles of use", Fertilite Contraception Sexualite 26 (4) :291-6
  40. Hilgers TW na JB Stanford ((1998) "Creighton Model NaProEducation Technology for avoiding pregnancy. Use effectiveness", Journal of Reproductive Medicine 43(6):495-502
  41. 41.0 41.1 [77] ^ oward, M.P. and Stanford, J.B. (1999) "Pregnancy probabilities during use of the Creighton Model Fertility Care System" Archives of Family Medicine 8 (5) :391-402
  42. "Natural contraception 'effective'", BBC News, 2007-02-21. Retrieved on 2007-09-25. 
  43. James Trussell et al. (2000) "Contraceptive effectiveness rates", Contraceptive Technology - 18 Edition, New York: Ardent Media. On-press.
  44. Ryder R (1993). ""Natural family planning": effective birth control supported by the Catholic Church". BMJ. 307 (6906): 723–6. doi:10.1136/bmj.307.6906.723. PMC 1678728. PMID 8401097.
  45. Hilgers T, Daly K, Prebil A, Hilgers S (1992). "Cumulative pregnancy rates in patients with apparently normal fertility and fertility-focused intercourse". J Reprod Med. 37 (10): 864–6. PMID 1479570. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  46. Wang X, Chen C, Wang L, Chen D, Guang W, French J (2003). "Conception, early pregnancy loss, and time to clinical pregnancy: a population-based prospective study". Fertil Steril. 79 (3): 577–84. doi:10.1016/S0015-0282(02)04694-0. PMID 12620443.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  47. Nouriani, Mory (Mei 2006). Infertility (PDF). National Women's Health Information Center, U.S. Department of Health and Human Services, Office on Women’s Health. uk. 2. Iliwekwa mnamo 2007-06-08.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) . "Some signs that a woman is not ovulating normally include irregular or absent menstrual periods."
    [75] "A woman who is not ovulating normally may have irregular or missed menstrual periods."
    [76] "If you have an irregular cycle there is a good chance you are not ovulating normally."
  48. Ellington, Joanna (2004). "Sperm Transport to the Fallopian Tubes". Frequently Asked Questions with Dr. E. INGfertility Inc. Iliwekwa mnamo 2008-04-27.
  49. [95] ^ Weschler (2002), uk. 173.
  50. [96] ^ Weschler (2002), uk.316
  51. [97] ^ Weschler (2002), uk.3-4 ,155-156, Insert p.7

Tazama Pia

  • Lunaception