Bahari ya Okhotsk : Tofauti kati ya masahihisho

Majiranukta: 55°N 150°E / 55°N 150°E / 55; 150
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Created by translating the page "Sea of Okhotsk"
(Hakuna tofauti)

Pitio la 19:35, 10 Oktoba 2019

55°N 150°E / 55°N 150°E / 55; 150

Ramani ya Bahari ya Okhotsk

Bahari ya Okhotsk ni bahari ya pembeni ya Pasifiki ya magharibi. [1] Iko kati ya rasi ya Kamchatka upande wa mashariki, visiwa vya Kurili upande wa kusini mashariki, kisiwa cha Hokkaidō upande wa kusini, kisiwa cha Sakhalin kwenye magharibi, na pwani ya Siberia ya mashariki upande wa magharibi na kaskazini. Ghuba ya Shelikhov iko upande wa kaskazini mashariki. Jina limetokana na mji wa Okhotsk ambayo ni mji wa kwanza ulioundwa na Warusi katika Mashariki ya Mbali .

Jiografia

Hifadhi ya Kitaifa ya Shiretoko kwenye pwani ya Hokkaido, Japan

Eneo la Bahari ya Okhotsk km2 1,583,000. kina cha wastani ni mita 859, kina kikubwa kina urefu wa mita 3,372. Imeunganishwa na Bahari ya Japani upande wa magaribi kupitia Ghuba ya Sakhalin, upande wa kusini kupitia mlangobahari wa La Pérouse.

Katika msimu wa baridi, usafiri kwenye Bahari ya Okhotsk unakuwa mgumu, au hata haiwezekani, kwa sababu ya uwingi wa barafu.

Visiwa

Baadhi ya visiwa vya Bahari ya Okhotsk ni kubwa kiasi. Hii ni pamoja na Hokkaido ambayo ni kisiwa cha pili kwa ukubwa cha Japan, na Sakhalin ambayo ni kisiwa kikubwa cha Urusi. Visiwa vingi vidogo vya bahari hii havina wakazi hivyo ni maeneo bora ya kuzaliana kwa sili na pinipedia wa spishi mbalimbali pamoja na ndege wa baharini.

Bandari za maana

Hori ya Nagayevo karibu na Magadan, Urusi

Marejeo

  1. Kon-Kee Liu; Larry Atkinson (June 2009). Carbon and Nutrient Fluxes in Continental Margins: A Global Synthesis. Springer. ku. 331–333. ISBN 978-3-540-92734-1. Iliwekwa mnamo 29 November 2010.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)

Tovuti za Nje

Kigezo:Commons cat-inline