Nenda kwa yaliyomo

Maili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maili ni kipimo cha urefu. Si kipimo sanifu cha kimataifa SI bali ni kizio cha vipimo vya Uingereza. Zamani ilitumiwa sana lakini siku hizi matumizi yamepungua sana.

Maili si kipimo sanifu cha kimatifa hivyo urefu wa maili moja ni tofauti kati ya nchi na nchi hata kama ni maili ya nchi kavu au maili ya baharini.

Hadi leo inatumiwa katika nchi zinazotumia lugha ya Kiingereza ingawa hizi zote zinaelekea kubadilisha au zimeshabadilisha tayari kawaida yao kwa kutumia kilomita. Ila tu watu wamezoea maili sana wakiendelea kuitumia.

Maili ya Kiingereza ina futi 5,280 au mita 1,609.

Maili ya baharini ni mita 1,852.

Maili asilia

[hariri | hariri chanzo]

Asili ya maili ni kawaida ya Waroma wa Kale. Walitumia kipimo cha milia passuum (=hatua 1000) kwa kupima urefu wa mbali.

"Milia" hii ilikuwa sawa na futi za Kiroma 5,000. Kipimo hiki cha Kiroma kilingia katika vipimo vya mataifa ya Ulaya.