Mtumiaji:Sendi matiti
UTAWALA WA WANGOREME
[hariri | hariri chanzo]kawaida wangoreme walikuwa hawana utemi wa kimila ila kulikuwa na utemi wa utawala. Kabla ya watemi hao wangoreme walitawaliwa na Wakora Nyangi ambao walimaliza matatizo yote na waliogopwa sana. Watemi ambao wametawala ngoreme tangu Mjeremani ni kama ifuatavyo:
a. Mtemi Kichamri na Mairo Ichumbe (1932 – 1936)
Walitawala ngoreme kwa awamu moja yaani kila mtu na eneo lake. Kichamri alitawala eneo la Mwibara na Mtemi Mairo alitawala maeneo yote ya kando ya Mto Mara kuanzia Bumare hadi Borenga. Watemi hao walikuwa na sifa zifuatazo:- Mtemi Kichamri alipenda sana utukufu yaani yeye alikuwa anabebwa. Na Mtemi Mairo Ichumbe alikuwa msafi, lakini anayesisitiza taratibu zifuatwe kwa hali ile Wangoreme hawakumpenda hivyo liliundwa kundi la siri ambalo lilimhamisha kwa nguvu na kwenda Ikoma na kufia huko.
b. Mtemi Birage 1936 – 1937
Huyu alikuwa mtu mwenye nguvu na mnene sana, inasemekana aliweza kushikiria L/Rover na ikashindwa kuondoka, lakini hakusoma hata kidogo. Alidanganywa na Atanas na kutia dole gumba kwenye barua ambayo ilimuondoa madarakani bila kujua. Mzee Birage alitaka kupambana na Mzee Nyigana kwa mieleka, kabla ya zoezi hilo wakapewa jaribio la kula vyakula mbalimbali, hapo ndipo Mzee Birage alipoonyesha kuwa atamuumiza Mzee Nyigana kwani kibuyu cha togwa alikunywa chote bila kupumzika, ugali kisonzo alimega mara tatu akamaliza ugali uliomo. Hapo washauri ndipo walipozuia zoezi hilo. Mzee Birage alifanana na mtoto wake wa kike kwa nguvu, urefu na unene bahati mbaya mama huyo alifia huko Ikizu.
c. Mtemi Athanas 1937 - 1947
Yeye alikuwa siyo Mongoreme alikuwa Mkwaya aliletwa Ngoreme kama Karani wa Mtemi Birage. Kwa kuwa yeye alijua kusoma na kuandika alifanya mapinduzi ya ujanja. Aliandika barua kwa Bwana shauri wa kikoloni akieleza kuwa Birage amesema yeye hawawezi Wangoreme na hawezi kukomesha wizi hivyo afadhali Atanas ashike madaraka ya utemi. Na kweli barua hiyo ikakubalika, na D.C akaja na kumtangaza Atanasi kuwa Mtemi. Baada ya Mtemi Atanas kusimikwa utemi kweli alifanya kazi nzuri sana kweli alikomesha wizi, lakini kwa mateso makali sana kwa wananchi, mtu aliyehisiwa alipewa karai la kokoto au changarawe atafune kwa meno yake na alishinda juani. Pia alianzisha Amini (ekehore) ambayo ukihisiwa mwizi unawekewa maji yaliyochanganywa na dawa ndani ya fuvu la kichwa cha binadamu aliyekufa kwa ukoma. Baada ya mateso hayo ya muda mrefu na wizi kukomeshwa wananchi wengi walijenga chuki kwa Atanas hivyo kama ilivyokuwa kwa Mairo Ichumbe, Atanas naye aliundiwa kundi la siri ambalo liliongozwa na Nyamang’we Mayengo ambaye wakati huo alitoka vitani Burma mwaka 1947 Mtemi Atanas aliingiliwa na karibu vijiji vyote na kuhamishwa kwa nguvu kwenda Musoma. Baada ya kufaulu hilo wangoreme walikutana na D.C akisisitiza kuwa Mtemi Atanasi arudi lakini wangoreme walikataa na kusema yeyote watakayemleta nje ya wangoreme (kabila jingine) wao watamhamisha kama walivyofanya kwa Atanas. Baada ya D.C kuona hivyo alikubaliana nao na kuwataka wataje mtu toka kabila la wangoreme, wakatajwa watu wawili Simeona Nyichomba na Nyamang’we Mayengo walimchagua Simeon ambaye wakati huo alikuwa ni karani wa Mahakama huko Nyahuburi Tarime akashinda na kuwa Mtemi. Baadaye kwa kuenzi kazi ya Nyamang’we Mayengo ya kuandaa mkakati wa kumng’oa Atanas wangoreme walitunga wimbo ukisema “Nyamang’we hee, Nyamang’we hee niye wakona eniko ikagi gwita omukama” kwa tafasiri Nyamang’we, Nyamang’we wewe ndiye uliyeunda kundi la siri kwenda kuua Mtemi. Huo ndiyo ukawa mwisho wa utawala wa Mtemi Atanas ambaye alikuwa na mke wake aliyefahamika kwa jina la Tekela (Tecler). Ndiye aliyejenga shule ya Majimoto na Mahakama ya Majimoto. Pia kitu ambacho kiliongeza chuki kwa wangoreme dhidi ya Atanas, ni pale Atanas alipoiba fedha za makusanyo (Ekehenda) na kusingizia watu fulani fulani kuwa wao ndiyo wezi. Serikali ilipotuma mtu aitwaye Chonachona (Mnusaji) wakati anaelekea kwa Chacha Mwirabi ambako pesa hizo zilifichwa, Mtemi Atanas alimkemea Chona na kusema hili halina uwezo wa kunusa na hivyo kumrudisha Majimoto bila mafanikio ya kupata hizo fedha.
d. Mtemi Simeon Nyichomba 1947 – 1963
Huyu ndiye mtemi aliyetawala kwa kipindi kirefu na aliyependwa sana na watu alikuwa siyo mkandamizaji, ila alipenda rushwa yeye alikuwa anasema wazi kuwa “ARABA TARENTA RIKUMBATI” “Tafasiri ndugu yangu lete tumbaku” na kesi inamalizika. Alileta sana maendeleo kwani katika kipindi chake shule, zahanati Marambo na barabara vilijengwa.
Zahanati: ya kisaka 1948, Majimoto 1947 na Kemgesi Shule: Kisaka, Nyagasense, Nyiboko, Nyabehore na Kemgesi Barabara: Toka Sirorisimba hadi Nyiboko. Marambo: Nyiboko, Borenga, Buchanchari, Nyamihangate, Nyansurumunti, Nyabehore, Mwimwamu na Kemarambo/Kikora Mtemi Simeon aliwapenda sana watu wake na yeye kupendwa sana. Baada ya sheria ya kufuta vyeo vya Ma – Chief na kutungwa. Mtemi Simeo alikuwa miongoni mwa watemi waliostafishwa na hapo kuwa mwisho wa utawala wake, alifariki 1964 akiwa ameoa wanawake wanne ambao ni Mkami Mahende, Nyambori, Kimori na Nyamang’ondi. Mtemi Simeon alikuwa na mwandiko mzuri sana, hata sasa yako katika makitaba ya chuo kikuu cha DSM, chumba cha kumbukumbu (Special Reserve). Mtemi Simeoni alikuwa akipita na kuwakuta watu husimamisha gari lake aina ya L/Rover na kuwasalimia, na watu hao walimnyenyekea sana, wakipokea salamu zake kwa kusema “Kasinge, kasinge, neku ntigeoho” “Tafasiri Mkuu, mkuu nife mimi kabla ya wewe”. Jina kamili la Simeon ni Simeon Clement Mapesa Nyarang’anya.