Mtumiaji:Halima Nurdin Mwadau
Mandhari
Ninaitwa Halima Nurdini Mwadau. Mwanafunzi wa shahada ya awali katika Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro. Ninapenda sana kusoma makala na vitabu mbalimbali vya hadithi fupi, Riwaya pamoja na Tamthiliya.
Usomaji wa vitabu na makala mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa, huwa na mchango mkubwa katika kuinua na kupevua uwelewa wa watu wapendao kujifunza.
Baadhi ya watu hususani vijana hawana ratiba maalumu za kudurusu makala na vitabu kwa lengo la kujifunza badala yake hujikita zaidi katika mambo yasiyofaa au yasiyo na tija kwao na hata vizazi vyao.
Napenda kutoa rai kwa vijana na jamii kwa ujumla, kuweka ratiba za kujisomea makala na vitabu ili kupanua maarifa zaidi na zaidi.