Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Kalenda ya Juliasi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Julius Caesar au Juliusi Kaisari?

[hariri chanzo]

Ndesanjo, nina mashaka na masahihisho kadhaa uliyafanya katika makala hii.

Kwanza jambo la "Kalenda ya Mwezi" au "mbalamwezi". Ninavyoelewa "mbalamwezi" inataja nuru ya mwezi hasa wakati wa mwezi mkubwa au mpevu ukiwa na mwanga mwingi.(taz. Kamusi ya Kiswahili sanifu, pia Johnson). Lakini kalenda ya mwezi inataja tabia ya kalenda kufuata mwendo wa mwezi wote; kwa kawaida kalenda hizi zinatumia kinyume cha mbalamwezi kugawa vipindi vya miezi yaani mwezi mwandamo. Tena kuna makala ya "kalenda ya mwezi" na kiuongo chake kimepotea sasa. Kuna sababu nzuri ambayo sijaelewa bado? Menginevyo naona "mbalamwezi" ni kosa.

Halafu Julius Caesar au Juliusi Kaisari. Ulitaka kurudia alivyotafsiri Nyerere? Kwanza hakutafsiri "Juliusi" lakini "Julius". Sioni faida kuongeza "i" kwa neno lolote. Ni jambo la kawaida lakini hakuna lazima.

Halafu Kaisari - Caesar. Labda angalia makala ya "Kaisari" pia "Julius Caesar". Hapa tunahitaji mapatano. Tufanyeje tukiongeza makala ya kihistoria? Mimi naona afadhali tutumie majina halisi. Hasa katika mfano huo tukiwa na "Kaisari" kama cheo katika historia ya Tanzania wakati wa ukoloni, pia historia ya Ujerumani na Ulaya wa jumla. Halafu tunaye huyu mtu wa kihistoria Julius Caesar.

Nimeandika tofauti na Nyerere. Lakini nafikiri kama Nyerere angalikuwa na nafasi ya kuandika zaidi angalifika kwenye swali lilelile.

Kuhusu Ruma-Rumi: kuna yote mawili katika Kiswahili (tazama makala "Roma"). Je kuna faida gani kuisahihisha? Ukifanya hivyo naomba heri uweke pia redirect za kutosha.

Nitasubiri siku mbili jibu lako. Kama hakuna naona afadhali nirudishe lugha ya awali. --Kipala 00:56, 16 Aprili 2006 (UTC)[jibu]

Samahani kwa kuchukua muda. Ni kwakuwa sikuona jambo kubwa la kupinga katika hoja zako. Ingawa hakuna ubaya kutumia majina halisi, kuna majina ambayo tayari yamezoeleka kwenye Kiswahili. Kwa mfano, Yesu (sio Jesus), Yohana Mbatizaji (sio John the Baptist), Mtume/Mtakatifu Paulo (sio Saint Paul), n.k. Kuhusu Roma/Rumi. Tatizo ni kuwa ukisema Roma kunakuwa na utata wa maana kwani jiji la Rome ni Roma. Wakati "roman empire" imezoeleka kama kwa jina "Rumi."

Ni haya kwa sasa. --Ndesanjo 5 Mei 2006

Masahihisho

[hariri chanzo]

A) Nimefuta sentensi juu ya kalenda ya Kiethiopia. Haina uhusiano na kalenda ya Juliasi. Tofauti ya miaka imetokana na kadirio la Annianus Mwalexandria (badala ya kadirio ya Dionysius Exiguus) - tazama [[1]]

B) Nimerudisha jina la Julius Caesar badala ya "Kaisari Juliusi". Ugumu niliona kwa sababu makala yenyewe inasema Augusto alikuwa Kaisari ya kwanza. Katika Kiswahili "Kaisari" ni cheo cha mfalme mkuu - Caesar ni jina la mtu ambaye hakuwa na cheo hiki. Ni kweli ya kwamba jina ni asili ya cheo (taz makala "Kaisari") na pia waandishi kadhaa walijaribu kumtafsiri "Caesar" kwa "Kaisari" - kwa mfano Nyerere. Lakini hata Nyerere angeona tatizo kama angeendelea kuandika kuhusu habari za Warumi wa Kale. --Kipala 17:27, 9 Septemba 2006 (UTC)[jibu]