Sentimita ya ujazo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sentimita za ujazo)
Kikombe cha upimaji chenye sentimita ya ujazo 1000, sawa na lita 1 ya maji

Sentimita ya ujazo ni kipimo cha mjao chenye urefu, upana na kimo cha sentimita moja na kiwango katika vipimo vya SI. Kifupi chake ni cm³.

Kuna sentimita za ujazo 1,000 ndani ya mita ya ujazo. Kwa hiyo 1 cm³ ni sawa na mililita moja (kifupi: ml).

Kiasi hiki cha maji kina uzito wa gramu moja.