Nenda kwa yaliyomo

Semaglutidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Semaglutide)

Semaglutidi (Semaglutide), inayouzwa kwa majina ya chapa ya Ozempic miongoni mwa mengineyo, ni dawa inayotumika kutibu Kisukari aina ya 2 na unene uliokithiri.[1] Haipendekezwi sana kuliko metformin, ingawa zote mbili zinaweza kutumika pamoja.[1][2] Dawa hii inaboresha udhibiti wa sukari ya damu, hupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo, na kupunguza hatari ya matatizo ya figo.[1] Inatumika kwa kupitia mdomoni au kwa kudungwa sindano chini ya ngozi.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, kutapika, kuhara, maumivu ya tumbo, na kuvimbiwa choo.[1] Madhara yake makubwa yanaweza kujumuisha ugonjwa wa kisukari wa asidi nyingi damuni (<a href="https://simple.wikipedia.org/wiki/Diabetic_ketoacidosis" rel="mw:ExtLink" title="Diabetic ketoacidosis" class="cx-link" data-linkid="176">diabetic ketoacidosis</a>), sukari ya chini ya damu, na kongosho.[2] Kuna wasiwasi kwamba matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto, na kutumia wakati wa kunyonyesha hakupendekezwi.[1] Dawa hii inafanya kazi kama glukagoni ya kibinadamu iliyo kama peptidi-1 (GLP-1) na huongeza kutolewa kwa insulini, inapunguza kutolewa kwa glukagoni, na kupunguza uondoaji wa votu tumboni.[2]

Semaglutidi iliidhinishwa kwa matumizi ya matibabu nchini Marekani katika mwaka wa 2017.[1] Iliundwa na shirika la Novo Nordisk[1] na ilikuwa GLP-1 ya kwanza ambayo inaweza kuchukuliwa kupitia njia ya mdomo. Nchini Uingereza, miligramu mbili za sindano iligharimu Huduma ya Taifa ya Afya (NHS) takriban £73 kufikia mwaka wa 2020.[2] Kiasi hiki nchini Marekani kiligharimu takriban Dola 850 kufikia mwaka wa 2021. [3]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Semaglutide Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). American Society of Health-System Pharmacists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 2 Aprili 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 BNF (tol. la 80). BMJ Group and the Pharmaceutical Press. Septemba 2020 – Machi 2021. uk. 738. ISBN 978-0-85711-369-6.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: date format (link)
  3. "Ozempic Prices, Coupons & Savings Tips". GoodRx (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 16 Aprili 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)