Newfoundland
Newfoundland (far. Terre neuve) ni kisiwa kikubwa cha Kanada katika Bahari Atlantiki. Eneo lake ni kilomita za mraba 108,860 kuna wakazi wapatao 479,538. Pamoja na maeneo kwenye bara ni sehemu ya jimbo la Kanada linaloitwa Newfoundland na Labrador. Mji mkuu ni St. John's kwenye rasi ya Avalon.
Jina lamaanisha "Nchi Mpya", kikamilifu "nchi iliyokutwa sasa karibuni" ambalo ni maana ya jina "newe founde islande" lililoandikwa na nahodha John Cabot aliyetunga ramani ya kwanza ya kisiwa hiki.
Wakati wa karne ya 17 wavuvi Wafaransa na Waingereza walivutana kwa sababu ya uwingi wa samaki katika bahari karibu na kisiwa. Wengine walijenga makazi kwenye pwani. Sehemu ya Maindio wazalendo walikufa kutokana na magionjwa mapya kutoka Ulaya, lakini sehemu nyingine ilibaki, wako hadi leo.
Tangu 1713 Uingereza ilishinda na kupata mamlaka juu ya ksiwa chote. Katika karne ya 19 wahamiaji wengi kutoka Eire, Uskoti na Skandinavia iliongeza idadi ya walowezi kutoka Ulaya. Biashara ilistawi kutokana na uvuvi. Reli ya kwanza ilijengwa mwaka 1882. Eisenbahnlinie über die Insel gebaut.
Kuanzia 1825 Newfoundland ilikuwa koloni ya Uingereza pekee na Kanada ikaendelea kuwa nchi ya kujitawala ndani ya milki ya Britania. Ni 1948 iliamua kujiunga na Kanada.