Nenda kwa yaliyomo

Muna Lee (mwandishi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Muna Lee(mwandishi))

Makala hii kuhusu mwandishi mwenye makao yake Pwetoriko. Kwa mwanamichezo wa Marekani,angalia Muna Lee (mwanamichezo).

Muna Lee
Alizaliwa: 29 Januari 1895(1895-01-29)
Raymond, Mississippi, Marekani
Alikufa: 3 Aprili 1965 (umri wa miaka 70)
San Juan, Puerto Rico
Kazi: Mshairi, Mwandishi
Aina: Pan-Amerika,Haki za wanawake, Riwaya za upelelezi za kubuni

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Muna Lee (29 Januari 1895 - 3 Aprili 1965) alikuwa mwandishi na mshairi wa Marekani ambaye alikuwa anajulikana sana kwa maandishi yake yaliyokuza sera za Pan-Amerika na sera za kuwapa majukumu makubwa wanawake.

Alizaliwa Raymond, katika eneo la Mississippi, Lee alianza kazi yake ya kuandika kama mshairi maarufu. Alikuwa mtu anayetafsiri na mtetezi wa maandiko ya Amerika ya Kilatini, alichangia kwa njia kubwa sana katika fasihi ya kisasa ya Pan-Amerika.


Bendera ya Puerto Rico

Akiwa kiongozi wa kupigania haki za wanawake, Muna Lee alifanya mchango muhimu katika harakati za kisasa za wanawake, hasa mapambano ya haki sawa. Alikuwa mwanzilishi wa Tume ya Wanawake ya Amerika Zote. Ilikuwa katika jiji la New York, alikokutana na mume wake wa baadaye, mshairi wa Puerto Rico na mwandishi wa habari aliyeitwa Luis Muñoz Marín, ambaye angekuwa gavana wa kwanza wa Pwetoriko wa kuchaguliwa kwa uchaguzi wa kidemokrasia. Walifunga ndoa mnamo tarehe 1 Julai 1919 na wakati wa muungano wao walikuwa na watoto wawili: binti mmoja Munoz Muna Lee (anayejulikana kama Munita) na mwana mmoja Luis Munoz Lee. Muna alipewa talaka rasmi mnamo 15 Novemba 1946, miaka miwili kabla ya Luis Muñoz Marín kuandikwa katika vitabu vya historia alipochaguliwa kama gavana. Iwapo wangekuwa bado mume na mke, Lee angekuwa Mwanamke wa Kwanza wa kwanza wa kisiwa hicho cha Pwetoriko.

Kutoka mwaka wa 1934-1938, Lee aliandika riwaya tano za upelelezi chini ya jina la Newton Gayle(akimshirikisha Maurice Guiness). Riwaya hizo zilipaata sifa na umaarufu wakati huo hasa kwa matumizi ya mazungumzo ya lugha mbili,zimetafsiriwa katika lugha za Kiitaliano na Kifaransa.

Mwaka wa 1941, alijiunga na Idara ya Marekani kama mtaalamu katika masuala ya tamaduni za Amerika. Yeye aliaga dunia kwa kuugua na saratani ya mapafu mnamo tarehe 3 Aprili 1965 huko San Juan, Pwetoriko. Alizikwa katika Santa Maria Magdalena de Pazzis katika eneo la Old San Juan.

Angalia Pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]