Mtandao wa simu za rununu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kilele cha mnara wa mtandao wa simu
Seli za ndani nchini Ujerumani

Mtandao wa simu za rununu ni mtandao wa simu ambapo kiunga cha mwisho hakina waya.

Mtandao huo unasambazwa juu ya maeneo ya ardhi yanayojulikana kama "seli", kila moja ikihudumiwa na kipokeleo cha eneo husika lakini aghalabu huwa likihudumiwa na vituo pokezi msingi vitatu. Vituo hivyo pokezi msingi hutoa huduma ya mtandao kwa seli, yaani eneo husika, ambapo huduma hiyo hutumika katika usambazaji wa mawimbi ya sauti, data pamoja na aina nyingine za taarifa. Kila seti ya seli husika hutumia masafa tofauti kutoka kwa seli jirani, ili kuzuia mwingiliano wa masafa na kutoa huduma ya uhakika kwa kila seli.