Msaada:Jamii
Jamii (kwa Kiingereza: category) ni namna yetu ya kupanga makala kwa makundi. Ukiweka matini [[Jamii:JINA-LA-JAMII]] chini kabisa kwenye makala fulani, programu ya MediaWiki itaonyesha jamii hiyo chini ya makala hiyo na kuunda "ukurasa wa jamii" tunapokuta orodha ya makala zote zenye alama hiyo.
Kurasa hizo za jamii zinasaidia kuangalia makala zinazohusiana.
Mara nyingi makala itakuwa na jamii zaidi ya moja.
Mfano: Watu. Mtu ataingizwa katika jamii za raia wa nchi fulani, jamii ya watu wenye kazi au fani fulani, jamii ya watu waliozaliwa mwaka fulani, kama ameshaaga dunia jamii ya watu waliofariki mwaka fulani.
Mfumo wa jamii
Jamii zote huunganishwa katika mfumo wa jamii. Mfumo huu unatofautisha jamii za juu na jamii za chini. Ngazi ya juu iko Jamii:Jamii Kuu; kutoka hapa unaweza kupeleleza kuna nini ndani ya jamii za juu. Mfano utaona jamii ya ngazi ya kwanza "Sayansi", ndani yake iko "Jiografia", ndani yake unapata nchi, mabara, miji na kadhalika.
Njia nyingine ya kuangalia mfumo ni kwenda Kurasa maalum (kwenye menyu ya kila ukurasa upande wa kushoto) na kuangalia "Orodha za kurasa", halafu kufungua Mfumo wa Jamii. Hapo ukiandika jina la jamii, utaona vijamii chini yake.
Kuteua jamii
Ukitafsiri makala kutoka Kiingereza, inafaa kuangalia jamii zilizopo kwa Kiingereza. Wakati mwingine utateua jamii kadhaa lakini unaweza pia kutumia jamii zote. Hapo unahitaji kufanya kazi mbili:
Kutumia jamii zilizopo
Angalia katika mfumo wa jamii kama jamii husika za Kiswahili ziko, halafu kuziandika chini ya makala kwa umbo la [[Jamii:JINA-LA-JAMII]]
Kuunda jamii mpya
Kama jamii ya Kiswahili haiko bado, utaanzisha jamii mpya kwa kuweka [[Jamii:JINA-LA-JAMII]] chini yake.
Kuunganisha jamii mpya
Hapa unatakiwa kuunganisha jamii mpya kwa ngazi ya juu, labda pia kwa ngazi 2 za juu. Kwa hiyo kama makala yako ni kuhusu mwimbaji wa nchi fulani, na hakuna jamii bado, utaunda kwanza [[Jamii:WAIMBAJI WA NCHI FULANI]]. Hii utahitaji kuunganisha na [[Jamii:WATU WA NCHI FULANI]]; kama ile haiko bado, basi unaiunda na kuunganisha na [[Jamii:NCHI FULANI]] .
Halafu utangalia pia mfumo wa jamii za fani (kazi), yaani kuunganisha [[Jamii:WAIMBAJI WA NCHI FULANI]] na [[Jamii:Waimbaji nchi kwa nchi]]. (ndani ya jamii hiyo za nchi kwa nchi unatumia namna ya kupanga A-B-C kwa kuandika [[Jamii:Waimbaji nchi kwa nchi|HERUFI YA KWANZA YA NCHI]].