Nenda kwa yaliyomo

Mali (kipindi cha runinga)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya kipindi cha MALI
Nembo ya kipindi cha MALI
Wahusika Wakuu wa kipindi cha MALI
Wahusika Wakuu wa kipindi cha MALI

Mali ni kipindi cha runinga kinachorushwa na stesheni ya NTV (Kenya). Wito wake kwa Kiingereza ni "United by Blood: Divided by Greed" (Kuunganishwa kwa damu; kutenganishwa kwa tamaa). Mali ilianza kurushwa nchini Kenya halafu nchini Uganda. Kipindi kilirushwa miaka 2011-2015.[1] Ki kipindi cha aina yake, huoneshwa mara tatu kwa wiki [2]

"Mali" inafuatilia maisha ya jamaa tajiri kabisa lakini inayosumbuliwa na mambo ya ndani. Mzee wa nyumba meoa wanawake zaidi ya mmoja na anaendesha nyumba yake kama kambi ya kijeshi.

Ndugu hao wanatofautiana kitabia, kitamaduni, kijamii na hali ya kimaisha lakini wote wanazo hadithi motomoto kuhusu mapenzi, pesa, nguvu, kutongozana na mafanikio.

Hadithi inachacha pale ambapo mzee wa nyumba, Bw. G Mali, anaanguka na kuaga dunia kabla ya kuwacha wasia. Anawacha jamaa mbili katika tamaa, ubatilifu, kugawanyika na pia kugunduliwa kwa siri nzitonzito za kijamaa na za kibinafsi.

Mali ni hadithi ya tamaa ya kufanya kinachofaa na mambo yote yanayohusu mwendo huo. MALI inapeleka mtazamaji katika mwendo wa kuonyesha dubwana za jamii hiyo, jamaa na umbali mtu anaweza kuenda katika kutafuta mapenzi, pesa na furaha iliyoje.

Mali inaonyesha upande mwingine wa utajiri pasi na ukweli wa jamaa waliotengana na njia tofauti kila ndugu anafanya ili kuiunganisha ilhali kuna tofauti nyingi.

Wahusika

[hariri | hariri chanzo]

Wahusika Wakuu

[hariri | hariri chanzo]

G Mali -George Ohawa

Mabel Mali -Mary Gacheri

Usha Mali -Mkamzee Mwatela

Bella -Carolyne Midimo

Nandi Mali -Mumbi Maina

Lulu Mali -Brenda Wairimu

Richard Mali -Kevin Samuel

Arthur Mali -Daniel Peter

Wahusika wadogo

[hariri | hariri chanzo]

Mwambu -Abel Amunga

Tony -Tonie Mwangi

Lucia -Kate Khasoa-Kole

Fadhili -Conrad Makeni

Don -Gerald Langiri

Bishop -David Gitika

Clara -Natasha Likimani

Zolo -Hamza Omar

Ron -Nic Wang’ondu

Nikita -Marilyn Perez

Miriam -Joan Arigi

Selena -Carolyne Ngorobi

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu kipindi fulani cha televisheni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mali (kipindi cha runinga) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.