Majadiliano:Duckie Thot

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Majadiliano:Duckie thot)

Duckie Thot: Maandishi ya koozeNyadak "Duckie” Thot alizaliwa tarehe 23 Oktoba mwaka 1995 mjini Melbourne katika nchi ya Australia. Wazazi wake walihamia Australia mwaka 1994 kutoka Sudani wakati wa vita. Wao ni Wasudani Kusini. Baba yake ni Daktari wa mifugo na mama yake anafanya kazi katika utunzaji wa watoto. Alikua na kaka na dada sita. Dada yake Nikki Thot ni mwanamitindo pia. Wakati akiwa mdogo, Duckie alikabiliwa na maswala mengi kama vile kudharauliwa kwa sababu ya ngozi yake nyeusi na jina. Aliamua kujipa jina la kisanaa "Duckie" kwa sababu jina hilo lilikuwa rahisi kutamka na wanafunzi wenzake na walimu vilevile. Duckie pia anaitwa “Black Barbie” kwa sababu yeye ni mrembo sana.

Kazi: Alipokuwa na umri wa miaka 17, Duckie aliwania taji la Australia’s Next Top Model. Akiwa katika mashindano, Duckie alikabiliwa na ukosoaji huo huo ambao aliokabiliana nao alipokuwa anakua. Wanamitindo wenzake walimwonea wivu sana kwa sababu ufuasi mkubwa aliokuwa nao. Katika mashindano, Duckie alijisuka nywele yake kwa sababu hapakuwa na msusi yeyote. Wasusi hawakuwa na ujuzi wowote wa kushughulikia nywele zake za asili za Kiafrika. Kwa sababu ya rangi yake ya ngozi, wasanii wa kiufundi walikuwa na ufahamu mdogo wa jinsi ya kumrembesha kwa kutumia foundation . Mwisho wa mashindano, alimaliza katika nafasi ya tatu. Baada ya mashindano, alihamia mjini Brooklyn katika jimbo la New York, nchini Marekani ili kuendeleza kazi yake. Yeye alipata umaarufu baada ya kushirikiana na Rihanna, mwanamuziki Mbarbados. Rihanna alimuajiri katika Savage x Fenty, kampuni ya mitindo. Baadaye, Kanye West alimuajiri katika Yeezy, kampuni ya mitindo pia. Duckie alifanya kazi kwa Victoria’s Secret pia. Utetezi: Duckie amekuwa akizungumza sana juu ya maswala ambayo wanawake weusi wanakabiliana nayo katika ulimwengu wa mfano, haswa wale walio na ngozi nyeusi kama yake. Katika mahojiano ya hivi karibuni alipoulizwa juu ya ubaguzi wa rangi katika tasnia ya kuigwa, alijibu, “Ubaguzi uko kila mahali. Lazima ujua jinsi ya kuupuuza.” Alifanya kazi kama Balozi wa L'Oréal, kampuni ya mrembo. Wakati wa Machafuko ya Sudani Kusini mwaka 2019, Duckie aliongea kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiuliza kuongezeka kwa ushiriki kwani Sudani Kusini ilikuwa kwenye mkutano wa vyombo vya habari wakati huo.

Maisha binafsi: Duckie ana ndugu zake sita wanaishi Melbourne, Australia. Katika Machi 2018, Duckie na Kofi Siriboe walitangaza kwamba walikuwa kwenye uhusiano. Kofi Siriboe ni mchezaji kutoka Ghana lakini alizaliwa Marekani. Katika Januari 2019, Duckie na Kofi walimaliza uhusiano wao. Yeye ni mtu wa kibinafsi na anajihusisha na mashabiki wake haswa kupitia Instagram yake.