Nenda kwa yaliyomo

Krimu ya urea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Krimu yenye urea)

Krimu iliyo na urea, pia inajulikana kama krimu iliyo na carbamidi, hutumiwa kama dawa na kutumika kwa ngozi kutibu ukavu na kuwasha kama vile inaweza kutokea kwa hali ya seli za ngozi kujikusanya na kutengeneza gamba na mabaka makavu yanayowasha (psoriasis), ugonjwa wa ngozi au ichthyosis.[1][2][3] Inaweza pia kutumika kulainisha kucha.[3]

Kwa watu wazima madhara yake kwa ujumla ni machache.[4] Mara kwa mara inaweza kusababisha kuwasha kwa ngozi.[1] Urea hufanya kazi katika sehemu hiyo kwa kulegeza ngozi iliyokauka.[5] Maandalizi yake kwa ujumla yana urea 5 hadi 50%.[2][3]

Urea iliyo na krimu imetumika tangu miaka ya 1940.[6] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni [7] na inapatikana kwenye kaunta.[3] Nchini Uingereza, gramu 100 ya krimu ya 10% hugharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban pauni 4.37.[2]

  1. 1.0 1.1 World Health Organization (2009). Stuart MC, Kouimtzi M, Hill SR (whr.). WHO Model Formulary 2008. World Health Organization. uk. 310. hdl:10665/44053. ISBN 9789241547659.
  2. 2.0 2.1 2.2 British national formulary : BNF 69 (tol. la 69). British Medical Association. 2015. ku. 796–798. ISBN 9780857111562.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 "Urea topical medical facts from Drugs.com". www.drugs.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Januari 2017. Iliwekwa mnamo 15 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Katsambas, Andreas; Lotti, Torello; Dessinioti, Clio; D'Erme, Angelo Massimiliano (2015). European Handbook of Dermatological Treatments (kwa Kiingereza) (tol. la 3). Springer. uk. 439. ISBN 9783662451397. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-16.
  5. "Urea Cream - FDA prescribing information, side effects and uses". www.drugs.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Januari 2017. Iliwekwa mnamo 15 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Loden, Marie; Maibach, Howard I. (1999). Dry Skin and Moisturizers: Chemistry and Function (kwa Kiingereza). CRC Press. uk. 235. ISBN 9780849375200. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-16.
  7. World Health Organization (2019). World Health Organization model list of essential medicines: 21st list 2019. Geneva: World Health Organization. hdl:10665/325771. WHO/MVP/EMP/IAU/2019.06. License: CC BY-NC-SA 3.0 IGO.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Krimu ya urea kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.