Hoteli ya Royal Palm (Miami)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Hoteli ya Royal Palm(Miami))
Hoteli yenyewe na ardhiinayoizunguka,1912

Historia[hariri | hariri chanzo]

Hoteli ya Royal Palm ni hoteli kubwa iliyoundwa na tajiri na mfanyibiashara wa reli,Henry Flagler,huko Miami,Florida. Ilipofungulia wageni milango yake mnamo mwaka wa 1897,Hoteli ya Royal Palm ilikuwa mojawapo wa hoteli za kwanza katika eneo la Miami. Jumba lenye magorofa tano na saluni katika sakafu ya sita, Hoteli ya Royal Palm ilikuwa ya kwanza mjini humo kuwa na vyumba vyenye stima,eleveta na dimbwi la kuogelea. Takriban miaka thelathini baadaye,Hoteli ya Royal Palm iliharibiwa na upepo mkali wa 1926 na ikaathiriwa na mchwa. Mnamo mwaka wa 1930,ilihukumiwa kuwa mbovu na kubomolewa kabisa.

Hoteli ilijengwa kwenye shamba la kijiji cha Tequesta. Mlima wa mchanga iliondolewa kufanyia njia ua la hoteli hiyo. Karibu fuvu 50 na 60 zilipatikana katika mlima huo na zikatupwa ndani ya mapipa. Baadhi ya fuvu hizo zilitolewa kama bidhaa za ukumbusho.

Dimbwi la Kuogelea ,1912

Mahali ilipokuwa[hariri | hariri chanzo]

Hoteli hii ilikuwa kando ya Mto Miami kwa upande wa Kaskazini. Ua la hoteli liliizunguka hotel, takriban sudusi ya maili moja kwa urefu. Hoteli hii ilisemekana kuwa "Ukoloni wa Kisasa", yenye sifa ya "pesa na mali". Kulikuwa na vyumba 450 ya wageni. Chumba cha wastani cha wageni kilikuwa na kipimo cha futi 12 na futi 18, na 100 vilikuwa na bafu ya kibinafsi. Chumba kuu cha maakuli kiliweza kuwa na wageni 500. Chumba cha pili cha maakuli kilikuwa cha aya na watoto. Kulikuwa,pia, na vyumba vya maakuli vya kibinafsi. Kulikuwa na vyumba vya michezo,chumba cha kusikiza nyimbo na densi ,vyumba 100 vya kuvaa nguo na dimbwi la kuogelea. Chumba cha kuchamsha maji,chumba cha kuunda umeme,chumba cha kufulia nguo na chumba cha kuunda barafu vilikuwa katika jengo tofauti. Hoteli ilikuwa na wafanyikazi 300, miongoni mwao kukiwa na wapishi kumi na sita. Ingawa katika mji wa Miami kulikuwa na kifungu cha sheria, kilichosisitizwa na Julia Tuttle,kilichokataa uuzaji wa vinywaji vileo pahali popote mjini humo,Hoteli ya Royal Palm ilikuwa na kibali cha kuuza vinywaji hivyo katika miezi mitatu ya misimu ya utalii.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Maelezo ya ziada[hariri | hariri chanzo]

1. Muir. P. 187

2. Muir. P. 65

3. Muir. Pp. 60, 70, 154

4. Rinhart. Pp.180-185.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]