Nenda kwa yaliyomo

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Hospitali ya Tumbi)

Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi, ilianzishwa kama Kituo cha Afya mnamo mwaka 1967, ikiwa na vitanda 35. Mwaka 1979 Kituo cha Afya kilipandishwa hadhi na kuitwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Kibaha.

Tarehe 16 Februari 1996, Hospitali ilitunukiwa jina la “Hospitali Maalum ya Tumbi”. Mwaka 2008, Hospitali Maalum ya Tumbi ilikuwa na vitanda 253 kwa ajili ya kulaza wagonjwa.

Hospitali Maalum ya Tumbi, ndiyo kubwa katika wilaya ya Kibaha, hivyo ilitunukiwa hadhi ya kuwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani mwaka 2011 ikiwa na vitanda 281. Inahudumia idadi kubwa ya watu 1,110,917 katika mkoa wa Pwani ikiwa inapokea wagonjwa 400-500 kwa siku.

Hospitali hutumika kama ngazi ya kwanza na ya pili pia inapata wagonjwa kutoka wilaya zote na mikoa ya jirani. Timu ya usimamizi wa hospitali ina wanachama msingi 12 na ina jukumu la kusimamia shughuli zote za kila siku na inaongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Afya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Hospitali katika Shirika la Elimu Kibaha.[1]