Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Hormozgan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Hormozgan)
Ngome ya Fort of Lady of the conception ndani ya kisiwa cha Hormozgan
Mahali pa mkoa wa Hormozgan katika Uajemi

Hormozgan (kaj ‏ هرمزگان‎) ni moja kati ya mikoa 31 ya Uajemi. Makao makuu yako mjini Bandar Abbas. Jina la mkoa hutokana na kisiwa cha Hormuz.

Mkoa huwa na wakazi 1,403,674 (sensa 2006). Eneo lake ni kilomita za mraba 70,669.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Hormozgan iko katika kusini ya Uajemi kwenye pwani la ghuba la Uajemi hasa sehemu ya mlango wa Hormuz. Ng'ambo la mlango wa Hormuz yako maeneo ya Oman na Maungano ya Falme za Kiarabu.

Mikoa jirani ni Bushehr, Fars, Kerman na Sistan na Baluchistan.

Eneo la mkoa huwa na sehemu mbili ambazo ni kanda nyembamba ya pwani pamoja na visiwa kwa upande mmoja na milima yabisi kwa upande mwingine. Pwani ni joto na unyevu anga ni juu. Waajemi wengi kutoka bara wanakuja hapa kwa likizo wakati wa baridi.

Makao makuu ya Hormozgan yako Bandar Abbas; miji nyingine ni Bandar Lengeh, Haji Abad, Minab, Qeshm, Jask, Bastak, Bandar Khamir, Gavbandi na Roudan.

Visiwa 14 katika Ghuba la Uajemi ni sehemu ya mkoa huu: