David Ben Gurion
David Ben Gurion (Kiebrania דוד בן גוריון; 16 Oktoba 1886; 1 Desemba 1973) alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa dola la Israeli.
Alizaliwa kwa jina la David Grün kwenye sehemu ya Poland iliyokuwa chini ya Milki ya Urusi katika familia ya Wayahudi waliojiunga na harakati ya Usioni. Mwenyewe alikuwa mfuasi wa Usioni na Usoshalisti.
Mwaka 1906 alihamia Palestina (wakati ule chini ya milki ya Osmani) baada ya kusikitika ubaguzi dhidi ya Wayahudi katika Milki ya Urusi. Alikuwa mfanyakazi wa kilimo mwanzoni akaendelea kuwa mwandishi wa habari na kujenga shirika ya walinzi kwa vijiji vilivyoundwa na Wayahudi waliohamia Palestian wakati ule. 1912 alikwenda Istanbul akachukua digri ya sheria kwenye chuo kikuu. Wakati ule alianza kutumia jina la Kiebrania "Ben Gurion" (maana yake mwanasimba).
Aliendelea kuwa kiongozi wa harakati ya kisoshalisti ya Wayahudi wasoshalisti alijenga chama cha wafanyakazi Wayahudi cha Histradut na pia kundi la wanamgambo wa Hagana lililoendelea baadaye kuwa kiini cha jeshi la Israeli.
Alikuwa kiongozi wa kisiasa na kijeshi wa Israeli katika vita ya kuanzisha nchi hii mwaka 1948/49 akatangaza uhuru wa Israel na kuwa kiongozi wa serikali ya kwanza.
Aliendelea kama waziri mkuu hadi 1963 alipojiuzulu lakini alishiriki katika siasa hadi 1970.
1973 aliaga dunia kwenye kibbuz Tel Hashomer.
Alihesabiwa kati ya watu muhimu 100 wa karne ya 20. Kiwanja cha ndege cha Tel Aviv imepewa jina lake kwa heshima.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu David Ben Gurion kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |