Nenda kwa yaliyomo

Bradley Carnell

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bradley carnell)

Bradley Neil Carnell, (amezaliwa 21 Januari, 1977) ni mchezaji wa mpira wa miguu pia ni kocha kutoka Afrika Kusini. Alicheza kama mlinzi na kwa sasa ni kocha mkuu wa St. Louis City SC ya Major League Soccer.

Kazi ya Mapema

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa mji wa Johannesburg, Carnell alihudhuria Shule ya sekondari ya wavulana Parktown huko Johannesburg. Alipokuwa kijana alicheza kwa timu za vijana za Southern Suburbs na Robertsham Callies kama mlinda lango na baadae alibadilishwa kuwa mlinzi.[1]

Kazi ya Uchezaji

[hariri | hariri chanzo]

Carnell alianza kucheza soka kitaalamu akiwa na umri wa miaka 16 mnamo 1993 akiichezea Bidvest Wits University. Alichezea pia timu ya Kaizer Chiefs (1997–98), VfB Stuttgart (1998–2003), na Borussia Mönchengladbach (2003–05). Mafanikio yake makubwa yalikuja Stuttgart ambapo alisaidia kushinda nafasi ya pili katika ligi mwaka 2003. Alikuwa miongoni mwa wachezaji waliochaguliwa kushiriki Kombe la Dunia la FIFA 2002.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bradley Carnell kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


.

  1. "Bio / Offering". bradleycarnell.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 28, 2014. Iliwekwa mnamo Aprili 5, 2014. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)