Nenda kwa yaliyomo

Bomu la ardhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bomu ardhini)
Bomu la ardhini la Vita Kuu ya Pili
Onyo la eneo penye mabomu ya ardhini yaliyobaki baada ya vita

Bomu la ardhini (ing. landmine) ni silaha inayofichwa ardhini na kulipuka wakati inaguswa au kusikitishwa na mwendo wa karibu.

Bomu la ardhini ni silaha ya utetezi inayotumiwa kuzuia au kuchelewesha mwendo wa adui karika eneo fulani.

Tangu vita kuu ya kwanza ya dunia mabomu ya ardhini yalitengenezwa viwandani na kupatikana kwa wingi. Tangi siku zile teknolojia ya mabomu haya yameendelea sana.

Kuna aina tofauti ambazo zinaweza kulenga hasa watu au magari kama kifaru. Wakati wa vita baridi Marekani na Urusi waliandaa pia mabomu ya nyuklia kwa matumizi ya bomu ardhini.

Mabomu ya ardhini yalisababisha kifo cha watu milioni 1 katika kipindi cha mika 30 iliyopita. wengi wao walikuwa watu raia, wanajeshi walikuwa asilimia 20 tu. Mara nyingi wantu wanauawa na mabomu ya ardhini baada ya mwisho wa vita kwa sababu ni silaha zilizofichwa na kusahauliwa baadaye. Ni hasa hatari kwa watoto wanaocheza au kwa wakulima.

Mabomu ya ardhini hazina gharam,a kubwa, zinatengenezwa kirahisi na sikazi kubwa kuzitega mahai pengi. Kwa hiyo wapagiganaji wasio na uwezo wa kununulia silaha ghali wanayapenda. Lakini hatari yao kubaki baada ya vita na kujeruhi au kuua watu miaka baada ya mwisho wa mapigano