Zumbe
Mandhari
Zumbe ni neno la Kisambaa linaloonyesha heshima na thamani ya mtu, ambalo maana yake halisi kwa Kisambaa ni Mfalme.
Kiongozi wa Wasambaa aliitwa Zumbe kama cheo chenye sifa kubwa kwa jamii hiyo. Huko Usambaa neno Zumbe pia hutumika kama salamu tangulizi unapogonga kwenye nyumba ya mtu kwa ajili ya kusalimia, yaani lazima utangulize zumbe kwa ajili ya heshima ya baba mwenye nyumba.
Katika siku za karibuni huko Usambaa, neno zumbe linatumika kumuonyesha mtu aliye na hali nzuri kimaisha au kimapato. Mfano mtu anapokuwa na hali zuri kimaisha Wasambaa kumuita zumbe, yaani wakimaanisha mtu mwenye heshima au anayethaminika katika jamii.
Asili ya neno ni cheo cha "jumbe" kwa Kiswahili kinachomtaja mkuu au mtawala wa kieneo.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zumbe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |