Yen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sarafu ya yen 10
Yen 1000

Yen ni pesa nchini Japani. Alama yake ya kimataifa ni ¥ lakini Japani penyewe huandikwa . Yen imekuwa pesa inayotumiwa sana duniani baada ya dolar na euro.

Pesa hii ilianzishwa mwaka 1871 na serikali ya Meiji ikifuata mifano ya pesa za Ulaya. Mwanzoni ililinganishwa na gramu 1.5 za dhahabu.

Thamani ya pesa ilishuka wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na baada ya vita kiwango chake kwa dollar ya Marekani kiliweka kwa ¥360 kwa US$1. Mwaka 2008 ilikuwa ¥104 kwa US$1.

Tangu kuimarika kwa uchumi wa Japani Yen imekuwa pesa muhimu duniani.

Kuna noti za Yen 1,000, 2,000, 5,000 na 10,000.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yen kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.