Them Mushrooms
Them Mushrooms ni kundi la muziki kutoka nchini Kenya lililobadilika baadaye jina lake kuwa "Uyoga"[1].
Staili zao ni hasa Chakacha, Benga pamoja na reggae. Kundi lilianzishwa 1972 na kaka 5 Teddy Kalanda Harrison, Billy Sarro Harrison, George Zirro Harrison, John Katana Harrison na Dennis Kalume Harrison. Waliobaki hadi leo ni Billy Sarro na John Katana walioungwa na wanamuziki wengine.[2]
Walikuwa maarufu kimaitaifa kwa wimbo wao Jambo Bwana (1980) uliorudiwa na waimbaji wengi Kenya, Tanzania hadi Ulaya ambako Boney M. waliutoa pia. Kwa jumla nakala zinazozidi 200,000 ziliuzwa.
Walianza kuimba kwenye hoteli za kitalii za Mombasa na pwani la Kenya na tangu 1987 walihamia Nairobi.[3]
Mwaka 2000 walipata tuzo la 'M-NET 2000 AWARD' linalotolewa na kituo cha TV cha Afrika Kusini M-NET Television Channel.
Baadhi ya Nyimbo zao Maarufu[hariri]
Them Mushroom walitoa albamu kadhaa.[4]:
- Jambo Bwana (1980) (Rocking in Africa / Greetings and Respect / Nyimbo Za Daktari / Madd Maddo Maddest / Lady / Oh Twaila / Jambo Bwana / Was 1st Lost Mama / What You See / Comment Allez-Vous / Come Stare / John Lennon / Ronja / Wanamziki Si Wakora) Jambo Bwana youtube
- Mama Africa (1983
- New Horizons (1985)
- At the Carnivore (1987
- Going Places (1988
- Almost There (1989
- Where We Belong (1990
- Zilizopendwa 91 (1991
- Zilizopendwa 92 (1992) Unkula Huu (chakacha) youtube
- Kazi Ni Kazi (1996) (Pongezi madereva wa matatu - youtube)
- Ni Hiyo (1998)
- Oh! Twalia]] (1998)
- Jambo Bwana (1999)
- Songs from Kenya (2000) (Jambo Bwana / Mushroom Soup / Wazee Wakumbuke / Wazee Wakatke / Zilizo Pendwa / Za Kale Zipo / Malaika / Wamsheba Wamsheba / Si Nguo / Kama Zamani / Hapo Kale)
- Zilizopendwa 2000 (2000)
- Uyoga (2004)
Viungo vya nje[hariri]
- ↑ Museke: Uyoga
- ↑ Uyoga - the Story
- ↑ Kenya: Journey through a rhythm nation, BBC News World: Africa. 30 Agosti 1999.
- ↑ I Big Q Entertainment Unlimited
| Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Them Mushrooms kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |