Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1924

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1924 ulikuwa wa 35 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 4 Novemba. Upande wa "Republican Party", Rais Calvin Coolidge (pamoja na kaimu wake Charles G. Dawes) aliwashinda mgombea wa "Democratic Party" John W. Davis (pamoja na kaimu wake Charles Bryan) na mgombea wa "Progressive Party" Robert La Follette (pamoja na kaimu wake Burton Wheeler).

Matokeo[hariri | hariri chanzo]

Coolidge akapata kura 382, Davis 136 na La Follette 13. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.