Sokrates
Sokrates (kwa Kigiriki Σωκράτης, Sōkrátēs, 470–399 KK) alikuwa Mgiriki (mtu wa Athens), mwanafalsafa. Anthony Gottlieb alimwita shahidi na mtakatifu wa falsafa (Monk & Raphael, 2000).
Nje ya falsafa, anajulikana hasa kwa kifo chake. Alifariki kwa ajili ya kunywa sumu kutoka mti wa “hemlok” baada ya kupatikana na hatia katika mahakama ya watu wa Athens. Ilidaiwa kwamba mafunzo yake yaliingilia dini ya mji wa Athens na yalipotosha vijana wake. Ingawa alipewa nafasi kutoroka ili kuepuka hukumu yake na kwenda uhamishoni, Sokrates alichagua kunywa sumu hiyo kwa sababu alikuwa amekubali kwa hiari yake afuate sheria za Athens, na akaamini kwamba angalikwepa hukumu yake angaliuaibisha mkataba huo.
Maarifa mengi kuhusu Sokrates yametokea mazungumzo yaliyoandikwa na Plato, mwanafunzi wake na mwanafalsafa, maandiko ya Zenephon, mtu wa rika lake, Aristofanes, na Aristotle. Kuna matatizo katika maandiko yanayomhusu Sokrates, hivyo sio vyema kutegemea chanzo kimoja tu. Ukitazama mambo yanayofanana baina ya maandiko, na ukaachilia mbali mambo yanayofikiriwa kuongezwa na mwandishi, Sokrates mwenyewe ataonekana.
| Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Ulaya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sokrates kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |