Siasa ya Cote d'Ivoire
Cote d'Ivoire |
Makala hii imepangwa kwa mfululizo: |
|
Nchi zingine · Atlasi |
Serikali ya Côte d'Ivoire (Ivory Coast) inachukua nafasi katika mfumo wa uwakilishi wa uraisi katika jamhuri ya kidemokrasia, ambapo Rais wa Cote d'Ivoire ni mkuu wa nchi na vilevile ni kiongozi wa serikali, na inafuata mfumo wa vyama vingi. Nguvu ya kiutendaji hutimizwa na serikali tu. Suala la utunzi wa sheria hutekelezwa kwa njia ya serikali yenyewe au bunge.
Mji mkuu rasmi tangu 1983 ni Yamoussoukro; hata hivyo, Abidjan unabaki kuwa kitovu cha utawala. Nchi nyingi huweka balozi zao mjini Abidjan, ijapokuwa baadhi yao (ikiwa ni pamoja na Uingereza) wamefunga harakati zao kwa sababu ya fujo zinaoendelea na ushambuliaji dhidi ya Wazungu. Wakazi wanaendelea kupata shida kwa kufuatia vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea.
Shirika la kimataifa la haki za binadamu limeng'amu matatizo ya uchukuliwaji mateka wa watu ambao si wapiganaji pande zote mbili na uchipukaji upya wa utumwa wa watoto katika uzalishaji ya kakao. Tangu tukio la 19 Septemba 2002, vita ya wenyewe ilivyoisha, na upande wa kaskazini wa nchi ukawa umechukuliwa na waasi, Vikosi Vipya (FN).
Uchaguzi mpya wa rais ulikuwa unatarajiwa ufanyika mnamo mwezi wa Oktoba 2005. Hata hivyo, uchaguzi huu mpya haukuweza kufanya kwa muda uliotakikana kwa kufuatia kucheleweshwa kwa maandalizi na ukaghailishwa hadi mnamo mwezi wa Oktoba 2006 baada ya makubaliano ya pande zote mbili za vyama hasimu kuafikiana. Baada ya uchelewesho wa muda mrefu, hatimaye uchaguzi ukafanyika mnamo 2010.
Vingo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |