Saa 72

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Saa 72 ni riwaya ya kikomando na kipelelezi inayoelezea mkasa wa makomandoo wa tano wanaotumwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ajili ya kumuua mbabe wa kivita ajulikanae kama Joseph Katanga aliyekuwa ameachiwa huru na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai na kurejea nchini Congo DRC na kuweka nia ya kugombea urais [1]

Katika riwaya hii iliyoandikwa mwaka 2018 na Japhet Nyang'oro Sudi kitengo cha kijasusi cha Ofisi Fukuzi kinamtuma mpelelezi wake makini mwenye uwezo mkubwa katika mapigano kwa ajili ya kwenda nchini Kongo kukamilisha kazi ya kumuangamiza mbabe huyo wa kivita ambae mwanzo walijua itakuwa ni kazi rahisi hasa wakiwatumia makomandoo wao ambao walijikuta wakiingia katika mtego mapema na kufeli misheni yao.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Sudi, Japhet Nyang'oro, 1981-. Saa 72 za kufa na kupona. Dar es Salaam. ISBN 978-9987-794-07-2. OCLC 1048027713. 
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Saa 72 kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.