Roki (mwanamuziki)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Rockford Josphat (alizaliwa Julai 7 1985) anayetambulika zaidi kwa majina ya jukwaani kama Roki au Rocqui, ni mwanamuziki wa kizazi kipya wa Zimbabwe, ambaye pia amejihusisha kwenye uigizaji. Kazaliwa Madagascar na kukuzwa ParkTown Waterfalls Harare, Roki alitengeneza mwanzo wake mwaka 2001 baada ya kutoa vibao kama vile "Seiko" ambaye ilishirikisha Leonard Mapfumo na Suzanna.

Anayejivunia umiliki wa "Msanii aliyeahidi zaidi kwa mwaka 2003", kupitia Tuzo za Taifa za Sifa za Sanaa za Zimbabwe(NAMA), Roki alitegeneza jina mwenyewe kama mtunzi wa nyimbo mwenye kipawa na muigizaji wa kipekee. Albamu yake ambaye ilibeba kibao kisichokufa "Chidzoka" ilishinda video bora ya mwaka na wimbo wa mwaka 2007.

Mwaka 2012, Roki alishiriki kwenye maonyesho ya Big Brother Africa 7, Yeye alipigiwa upatu kushinda, ila alienguliwa baada ya kuzozana na Mzimbabwe mwenzake wa nyumbani Maneta. Licha ya hii, Roki alijizolea umaarufu kwa taifa na kikanda.[1] Nyota huyo wa urban Grooves amezaa angalau watoto watano na wanawake tofauti, yeye aliacha shule akiwa na umri wa miaka 15. Nyimbo za Roki zimejikita katika mada za mapenzi, kifo, maisha na mgongano wa utamaduni wa Magharibi na Afrika.

Mtindo na mvuto[hariri | hariri chanzo]

Mtindo wa muziki wake inajumuisha Urban Groove, Soca, Dancehall, Afro-pop na Muziki wa Nyumbani. Mwaka 1996, wakati akiwa kwenye basi akiimba na marafiki, Roki alisikika na mwanamuziki wa hapa nchini ambaye alimwalika kutoa sauti za kuunga mkono wimbo wa mwanamuziki huyo.

Baadhi ya nyimbo zake inajumuisha Chidzoka, Ndokuda Gugu, Jordan, Zion, Ndoda, Mumwe, Suzanna and Nhliziyo.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Roki (mwanamuziki) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.