Ovid

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ovidi

Publius Ovidius Naso (* 20 Machi 43 KK - † mnamo 17 BK) anayejulikana kwa jina fupi la Ovid alikuwa mshairi wa Roma ya Kale. Alizaliwa Italia alipoishi hadi Kaisari Augusto aliamua kumwondoa katika Italia akapewa amri kuishi katika jimbo la Dacia (Romania ya leo).

Pamoja na Virgili na Horatius atazamiwa kama mmojawapo wa washairi wakuu wa Roma ya Kale. Mengi alichoandika yalihusu mapenzi.

Ukurasa wa kwanza wa toleo la Kiingereza la Ovid la mwaka 1632

Kazi za Ovid (tarehe za kutolewa)[hariri | hariri chanzo]

  • Amores ("mapenzi"), vitabu vitano, mnamo 10 KK
  • Metamorphoses, ("Mabadiliko"), vitabu 15, mnamo 8 BK.
  • Medicamina Faciei Feminae ("Sanaa ya Urembo"), mistari 100 imehifadhiwa, mnamo 5 KK.
  • Remedia Amoris ("Dawa la mapenzi"), kitabu 1, mnamo 5 KK.
  • Heroides ("Nyaraka za washujaa wa kike wa kale"), barua 21; barua 1-5 mnamo 5 KK; barua 16–21 mnamo 4 - 8 BK.
  • Ars Amatoria ("Sanaa ya mapenzi"), vitabu 3, mnamo 2 KK.
  • Fasti ("Sikukuu"), vitabu 6 kuhusu miezi 6 ya kwanza ya mwaka vyenye habari nyini juu ya kalenda ya Kiroma; vilikamilishwa mnamo 8 BK na kutolewa mnamo 15 BK.
  • Ibis ("Utakwenda"), shiri, mnamo 9 BK.
  • Tristia ("huzuni"), vitabu 5, mnamo 10 BK.
  • Epistulae ex Ponto ("Nyara kutoka Bahari Mweusi"), vitabu 4, mnamo 10 BK.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: