New England

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Boston ni moja kati ya miji mashuhuri sana ya New England.
New Hampshire
Cape Cod, Massachusetts

New England (Uingereza Mpya) ni jina la sehemu ya kaskazini-mashariki ya Marekani inayotazama pwani la Atlantiki. Katika eneo hili, kuna majimbo sita humu. Majimbo hayo ni pamoja na Maine, Vermont, New Hampshire, Massachusetts, Connecticut, na Rhode Island.


Historia[hariri | hariri chanzo]

Eneo hili lilikuwa chanzo cha ukoloni wa Uingereza katika Amerika ya Kaskazini. Mpelelezi mwingereza John Smith alitembelea nchi mnamo mwaka 1614 akatoa kitabu "A Description of New England" alipoeleza uwingi wa samaki, ubao na ardhi yenye rutba akisema nchi ilifaa kuunda "Uingereza Mpya" katika sehemu hizi. Maelezo yake yalianza kuvuta walowezi wachache walionunua ardhi kutoka kwa maindio wenyeji na kujenga makazi yao.

Tangu 1629 walowezi hao waliongezeka sana kutokana na uhamisho wa Wakristo waliowahi kujitenga katika kanisa rasmi la Uingereza na kuteseka huko. Walipewa nafasi ya kuhama Amerika walipoahidiwa uhuru wa kidini.

Walowezi walipanusha eneo lao ama kwa njia ya mapatano na wazalendo au kwa njia ya vita. Mara nyingi walowezi walianza kulima mashamba mapya nje ya sehemu za koloni ndogo za awali; kama walishambuliwa na wazalendo wasiokubali kulima kwao jeshi la miji ya koloni liliingia kati na kwa mdaasa wa silaha za Kiulaya kushinda makabila ya wenyeji. kwa njia hii maeneo ya walowezi yalipanuka polepole. Uwingi wa ardhi ya kulimia uliendelea kuvuta walowezi wapya na koloni hizi za Uingereza zilistawi kwa kuuza mazao kwenda Ulaya.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu New England kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.