New England
New England (Uingereza Mpya) ni jina la sehemu ya kaskazini-mashariki ya Marekani inayotazama pwani la Atlantiki. Katika eneo hili, kuna majimbo sita humu. Majimbo hayo ni pamoja na Maine, Vermont, New Hampshire, Massachusetts, Connecticut, na Rhode Island.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Eneo hili lilikuwa chanzo cha ukoloni wa Uingereza katika Amerika ya Kaskazini. Mpelelezi mwingereza John Smith alitembelea nchi mnamo mwaka 1614 akatoa kitabu "A Description of New England" alipoeleza uwingi wa samaki, ubao na ardhi yenye rutba akisema nchi ilifaa kuunda "Uingereza Mpya" katika sehemu hizi. Maelezo yake yalianza kuvuta walowezi wachache walionunua ardhi kutoka kwa maindio wenyeji na kujenga makazi yao.
Tangu 1629 walowezi hao waliongezeka sana kutokana na uhamisho wa Wakristo waliowahi kujitenga katika kanisa rasmi la Uingereza na kuteseka huko. Walipewa nafasi ya kuhama Amerika walipoahidiwa uhuru wa kidini.
Walowezi walipanusha eneo lao ama kwa njia ya mapatano na wazalendo au kwa njia ya vita. Mara nyingi walowezi walianza kulima mashamba mapya nje ya sehemu za koloni ndogo za awali; kama walishambuliwa na wazalendo wasiokubali kulima kwao jeshi la miji ya koloni liliingia kati na kwa mdaasa wa silaha za Kiulaya kushinda makabila ya wenyeji. kwa njia hii maeneo ya walowezi yalipanuka polepole. Uwingi wa ardhi ya kulimia uliendelea kuvuta walowezi wapya na koloni hizi za Uingereza zilistawi kwa kuuza mazao kwenda Ulaya.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Siasa
- New England Governors Conference
- New England Confederation Alliance Ilihifadhiwa 3 Agosti 2020 kwenye Wayback Machine.
- Historic
- Ramani
- Historic USGS Maps of New England & NY Ilihifadhiwa 5 Machi 2013 kwenye Wayback Machine.
- Map of New England. From the 1871 Atlas of Massachusetts by Walling and Gray.
- Mengineyo
- Flag of New England Ilihifadhiwa 1 Aprili 2007 kwenye Wayback Machine.
- New England Music Archive
- National Network of Libraries of Medicine - New England Region Ilihifadhiwa 30 Julai 2009 kwenye Wayback Machine.
- Hartford-Springfield Economic Partnership
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu New England kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |