Nematodi
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Nematodi | ||||||
|---|---|---|---|---|---|---|
![]() |
||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||
|
||||||
| Ngazi za chini | ||||||
Nematodi ni aina ya minyoo. Faila yao ni kati ya faila zenye spishi nyingi katika himaya ya wanyama.
Kutofautisha na kuainisha nematodi ni kazi ngumu. Hadi sasa spishi 80,000 zimeelezwa kitaalamu. Kuna makadirio ya kwamba idadi ya spishi inaweza kufikia nusu milioni. Nematodi wengi ni minyoo midogo myeupe au bila rangi inayoishi katika mazingira mabichi.
Kati ya nematodi wanaojulikana takriban spishi 15,000 ni kiparasiti yaani wanaishi ndani ya viumbe wengine. Spishi kadhaa husababisha magonjwa ya wanadamu. [1] Mlolongo wa DNA katika uchambuzi wa nematodi umepiga hatua sana, ikiwa ni pamoja na uhusiano wa spishi za miti.[2]
Marejeo [hariri]
| Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
