Nameless
David Mathenge (amezaliwa Agosti 1976), anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii Nameless, ni msanii wa kapuka nchini Kenya.
Taawasifu
[hariri | hariri chanzo]Yeye alipata umaarufu mwaka 1999 kupitia Ushindani wa "Star search" uliofanywa na stesheni ya radio ya [Capital(98.4 fm) http://www.capitalfm.co.ke], ambayo alishinda kwa wimbo wake wa awali "Megarider" Wimbo huu unaongelea m kijana ambaye hana pesa na ilhali anajaribu kumpata kipusa.Fedha alizonazo zinatosha tu tiketi ya Kenya Bus , na si maisha ambayo msichana huyo anataka. Alifanya wimbo huo na na mtayarishaji Tedd Josiah na ulikaa kwenya kwenye chati kwa wiki kadhaa Alitia saini na Ogopa Deejays mnamo mwaka wa 2001.katika Ogopa DJ's alikuwa pamoja na wasanii kama vile marehemu E-Sir amabaye walifanya wimbo wa "Boomba Train," na Amani : "Ninanoki" mwaka wa 2002 wimbo ambao ulivunja rekodi kwenya chati nchini Kenya kwa kusalia siku 110 nambari moja
Amekwenda kwenye ziara kaadhaa Afrika Mashariki , Marekani na pia Uingereza Alitoa albamu yake ya "on fire mwaka wa"2004. Pia mwaka huo huo wa 2004 Mathenge alimuoa msanii mwenzake Wahu Kagwe waliyekuwa wakirekodi pamoja katika Ogopa DJ's. Wana mtoto mmoja, binti ambaye alizaliwa mwaka 2006. Yeye pia ni mbunifu na alfuzu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.
Kikundi cha 'pop' kutoka Afrika Kusini ; Jamali walitoa wimbon wimbo wa "nigger" na ilisemekana kwamba waliuiba wimbo huo kutoka kwa Nameless. Lakini baadaye Jamali walikubali kumshirikisha Nameless kama Mwandishi wa "maisha" kwenye albamu yao ya "Yours Fatally"
Yeye alikuwa miongoni mwa orodha ya watu mia moja (100) wenya ushawishi mkubwa sana nchini Kenya kama iliyotolewa na gazeti la The Standard Agosti 2007 [1][2]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]- Kisima Music Awards 2004 - Mwanamziki wa Boomba Bora
- Kisima Music Awards 2006 - Mwanamziki Mwanaume Bora kwenya Afro Fusion & Video Bora (Sinzia) [3]
- 2006 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) - Mwanaume Bora (Kenya) [4]
- 2007 Tanzania Music Awards (Kilimanjaro Music Awards) - Wimbo Bora Afrika Mashariki (Sinzia) [5]
- 2007 Channel O Music Video Awards - Mwanaume Bora( "Sinzia") [6]
- 2008 Pearl of Africa Music Awards - Mwanaume mwanamziki Bora Kenya [7]
- Kisima Music Awards 2008 - Mwanamzikin Mwanaume wa Mwaka & Video Bora ( "Salari") [8]
- Tanzania Music Awards 2009 - Wimbo Bora Afrika Mashariki ( "Salari") [9]
- 2009 MTV Africa Music Awards - Msanii wa Mwaka, Chaguo la Wasikilizaji [10]
Kuchaguliwa
[hariri | hariri chanzo]- Tanzania Music Awards 2005 - Albamu Bora Afrika Mashariki ( "On Fire") [11]
- 2006 MTV Europe Music Awards 2006 - Mwanamziki Bora Afrika
- 2009 MTV Africa Music Awards - Mwanamziki Bora [12]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ The Standard, 21 Agosti 2007: 100 mest ushawishi Wakenya
- ↑ The Standard, 21 Agosti 2007: 100 mest ushawishi Wakenya - Entertainment
- ↑ "Kisima Awards winners 2006". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-04-08. Iliwekwa mnamo 2009-11-26.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help); Unknown parameter|https://web.archive.org/web/20090408174146/http://www.kisimaawards.co.ke/kminner.asp?cat=
ignored (help) - ↑ Ugandaonline.net: PAM Awards 2006 Winners
- ↑ Tanzania Music Awards: 2007 winners Ilihifadhiwa 2 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Museke: Channel O Music Video Awards 2007 winners Ilihifadhiwa 4 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Museke: PAM Awards Winners 2008 Ilihifadhiwa 18 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Kisima Music Awards: 2008 Kisima Music Awards Ilihifadhiwa 12 Desemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Daily Nation, Buzz Magazine, 12 Aprili 2009: The Kilimanjaro Awards 2009: The Highs na Lows Ilihifadhiwa 27 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Museke: MTV Africa Music Awards (MAMAs) 2009 winners
- ↑ "Tanzania Music Awards - Nominees 2005". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-05-15. Iliwekwa mnamo 2006-05-15.
- ↑ Museke: MTV Africa Music Awards (MAMAs) 2009 nominees Ilihifadhiwa 14 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine.
Viunganish vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ogopa DJs Tovuti rasmi Ilihifadhiwa 20 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.
- MTV Base Afrika profile: Nameless Ilihifadhiwa 10 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- Nameless 'profile, lyrics, audio, video, nk Ilihifadhiwa 8 Julai 2008 kwenye Wayback Machine.
- ya Capital