Nenda kwa yaliyomo

Namba kivunge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Namba kivunge (kwa Kiingereza composite number) ni namba asilia inayopatikana kwa kuzidisha namba tasa (prime numbers).

Kwa mfano namba 9 inapatikana kwa kuzidisha 3 kwa 3. Namba 12 inapatikana kwa kuzidisha 3, 2 na 2.

Namba asilia zote zinaweza kupangwa katika makundi mawili:

  • namba tasa
  • namba isiyo tasa kwa hiyo namba kivunge. Inapatikana kwa kuzidisha namba tasa, hata mara kadhaa jinsi ilivyoonekana katika mfano wa 12 hapo juu. Hii ni kati ya nadharia za kimsingi za hesabu.

Namba kivunge hadi 150

[hariri | hariri chanzo]

Namba kivunge hadi 150 ni kama zifuatazo:

4, 6, 8, 9, 10, 12, 14, 15, 16, 18, 20, 21, 22, 24, 25, 26, 27, 28, 30, 32, 33, 34, 35, 36, 38, 39, 40, 42, 44, 45, 46, 48, 49, 50, 51, 52, 54, 55, 56, 57, 58, 60, 62, 63, 64, 65, 66, 68, 69, 70, 72, 74, 75, 76, 77, 78, 80, 81, 82, 84, 85, 86, 87, 88, 90, 91, 92, 93, 94, 95, 96, 98, 99, 100, 102, 104, 105, 106, 108, 110, 111, 112, 114, 115, 116, 117, 118, 119, 120, 121, 122, 123, 124, 125, 126, 128, 129, 130, 132, 133, 134, 135, 136, 138, 140, 141, 142, 143, 144, 145, 146, 147, 148, 150.

Nyingi ni namba shufwa (tarakimu ya rangi nyeusi iliyokolea), idadi ndogo zaidi ni namba witiri. Sababu yake ni kwamba namba tasa zote ni witiri isipokuwa 2 yenyewe.

Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Namba kivunge kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.