Mtumiaji:Kipala/jaribio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msitu ni jumuiya ya mimmea mbalimbali, hasa miti

Msitu ni eneo kubwa penye miti mingi. Misitu inatofautiana kulingana na tabianchi na mazingira hivyo hakuna ufafanuzi kamili msitu uwe na ukubwa gani au idadi gani ya miti. Kwa hiyo haiwezekani kusema kikamilifu tofauti baina ya msitu na kijisitu.

Siku hizi takriban asilimia 30 za uso wa nchi duniani zimefunikwa kwa misitu; inakadiriwa ya kwamba zamani kulikuwa na nusu ya uso wa nchi duniani iliyokuwa na misitu. Misitu ni muhimu sana kwa ekolojia ya dunia na hivyo kwa uhai wote. Spishi nyingi za viumbehai vinategemea mazingira ya msitu, misitu inadhibiti dura ya maji kuanzia mvua hadi vyanzo vya mito na kulinda ardhi dhidi ya mmomonyoko. Misitu ina umuhimu kwa uchumi wa nchi.

Mazingira ya misitu[hariri | hariri chanzo]

Miti kwa jumla na pia misitu inahitaji mazingira fulani kwa ustawi. Kati ya masharti muhimu ni maji na joto la kutosha. Pasipo na usumbishaji, hasa mvua wa kutosha au baridi nyingi mno miti haistawi tena misitu haiko.

Mwisho wa msitu unaonekana hapa kwa kimo cha takriban mita 1900; mlima huu wa Alpi una kimo cha mita 2300

Kwa hiyo misitu haiko

  • penye tabianchi yabisi sana yaani katika hali ya ukame wa kudumu unaofanya nchi kuwa jangwa au nusu jangwa; pala ambako usimbishaji unaongezeka kidogo kuna miti kadhaa kama katika savana lakini maji haitoshi kwa kustawi kwa misitu.
  • Katika maeneo baridi ambako kipindi kinachopatikana kwa ukuaji wa miti kimepungua mno au hakipo. Miti kama mimea yote haiwezi kukua kama halijoto iko karibu na sentigredi 0 au chini yake kwa sababu maji ndani ya mmea yangeganda na kuharibu seli zake. Sehemu hizi ziko hasa katika mazingira yafuatayo
    • Tundra ya aktiki au antaktiki ambao halijoto hewani inafikia juu ya 0 °C kwa muda mfupi tu kila mwaka ilhali udongo unaendelea kugandishwa katika hali ya sakitu ya kudumu.
    • Milimani juu ya kimo fulani kinachotegemeana na mazingira; katika Alpi za Ulaya kimo cha miti ni mita 1800 - 2100 juu ya UB; kwenye mlima Kilimanjari ni mita 3000. Kuanzia kimo hiki baridi katika mwaka, mara nyingi pamoja na ukame, vinazuia ustawi wa miti.