Mkuu wa Serikali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mkuu wa serikali ni mtu aliye katika cheo cha pili katika utendaji wa nchi huru, dola la shirikisho au koloni. Yeye huongoza Baraza la Mawaziri. Cheo hicho hutofautiana na cheo cha mkuu wa dola kwa kuwa vyote vinaweza kuwa vyeo vya mtu mmoja au watu tofauti.

Katika serikali za kibunge na falme za kikatiba, mkuu wa serikali ndiye mwanasiasa kiongozi wa serikali na huwajibika kwa chumba kimoja cha bunge. Hata hivyo, yeye pia huripoti kwa mkuu wa dola.

Katika serikali za kirais na falme zisizo za kikatiba, mkuu wa serikali pia huwa mkuu wa dola.

Katika serikali za kikurugenzi, majukumu ya utendaji ya mkuu wa serikali hupatiwa kikundi cha wakurugenzi. Kwa mfano, Baraza la Shirikisho la Uswisi, ambapo kila mwanachama wa baraza huongoza idara fulani.

Majina ya cheo[hariri | hariri chanzo]

Waziri Mkuu ndilo jina la kawaida la cheo cha mkuu wa serikali. Majina yafuatayo pia hutumika: