Marzemino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Katika opera iliyoitwa Don Giovanni,Don Giovanni(mhusika mkuu) aliitisha glasi ya Marzemino kabla ya kuhukumiwa kwenda jehanamu

Marzemino ni divai nyekundu ya Italia iliyoundwa kutoka zabibu zinazopandwa katika eneo karibu na Isera, kusini mwa Trentino. Divai hii inajulikana sana kwa kutajwa kwake katika opera iliyoitwa Don Giovanni ya Wolfgang Amadeus Mozart (Versa il vino! Eccellente Marzemino!). Mzabibu huo huiva kama umechelewa na una urahisi wa kukabiliwa na magonjwa mengi ya zabibu,oidium ikiwa moja yao. Mvinyo uliotayarishwa kutoka kwa zabibu hizi una rangi nyekundu na weusi mdogo unaoutofautisha na divai nyinginezo na una ladha tofauti pia. Wanasayansi katika uwanja huu wa zabibu na mizabibu wanapendekeza kuwa asili ya zabibu hii ni kaskazini mwa Uitalia. Uchunguzi wa kisayansi wa mfumo wa DNA uliofanyika,katika kituo cha sayansi cha San Michele all'Adige,ulionyesha kuwa Marzemino ulikuwa na uhusiano wa uzazi na zabibu za Friuli-Venezia Giulia za Refosco dal Peduncolo Rosso na Teroldego. Huu ukawa ushahidi zaidi wa asili yake kuwa eneo lake.

Eneo la Trentino,Uitalia ambalo Marzemino hupandwa

Mikoa ya Mvinyo[hariri | hariri chanzo]

Marzemino unapatikana kote kaskazini mwa Uitalia hasa maeneo ya Lombardia,Veneto na Friuli-Venezia Giulia. Katika eneo la Lombardy,mara nyingi hutumiwa kama zabibu za kuchanganya na zingine kama Barbera, Gropello , Merlot au Sangiovese katika kuunda divai. Katika eneo la Trentino, Marzemino hutumika pia. Ingawa inaamanika kuwa na jukumu dogo katika historia ya Chianti,hivi leo haipatikani kwa urahisi katika eneo la Tuscany.

Upanzi wa mizabibu na utayarishaji divai[hariri | hariri chanzo]

Marzemino huwa na urahisi wa kuathirirwa na maradhi mbalimbali na pia huweza kuzalisha sana. Mzabibu huu unahitaji msimu mrefu wa kumea na huiva kwa kuchelewa. Marzemino inaweza kuzalisha divai nyepesi yenye ladha ya asidi kali kidogo. Katika hali ya anga baridi,ladha hiyo ya asidi inaweza kuonja kama nyasi na ladha ya matunda ya cheri. Baadhi ya mifano mitamu ya passito ya Marzemino,mara nyingi hutumika kuchanganywa na zabibu nyinginezo, inaweza kupatikana kote kaskazini mwa Uitalia.

Katika sanaa[hariri | hariri chanzo]

Katika opera iliyoitwa Don Giovanni, mhusika Don Giovanni anaitisha glasi moja ya Marzemino kabla ya kutupwa jehanamu. [7]

Visawe[hariri | hariri chanzo]

Marzemino inajulikana chini ya majina mbalimbali kote Uitalia. Majina haya ni kama Balsamina Nėra, Barzemin, Bassamino, Berzemino Calopico, Bossamino, Magnacan, Marsemina, Marzamino, Marzemin, Marzemino d'Isera, Marzemino Mataifa, Marzemino Padovano, Merzemina na UVA Tedesco.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. J. Robinson Vines, Grapes & Wines ukurasa wa 211 Mitchell Beazley 1986 ISBN 978-1-85732-999-5
  2. J. Robinson (ed) "The Oxford Companion to Wine" Toleo la tatu ukurasa wa 429 Oxford University Press 2006 ISBN 0198609906
  3. Oz Clarke Encyclopedia of Grapes ukurasa wa 122 Vitabu vya Harcourt 2001 ISBN 0151007144
  4. J. Kosman "THE SCENE: Wataalamu wakichagua divai"' San Francisco Chronicle 21 Juni 2002