Maryna Aleksiiva

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muogeleaji wa kisanaa na mshindi wa medali ya shaba ya Olimpiki Maryna Aleksiiva baada ya kupokea Zawadi ya Princess Olga Daraja la Tatu katika Ofisi ya Rais wa Ukraine huko Kyiv.
Muogeleaji wa kisanii Maryna Aleksiiva katika Ofisi ya Rais wa Ukraine

Maryna Antonivna Aleksiiva (alizaliwa Mei 29, 2001) ni muogeleaji kutoka Ukraine. Ni mshindi wa medali ya ubingwa wa dunia[1][2][3]. Maryna ni pacha wa Vladyslava Aleksiiva ambaye pia ni muogeleaji.

Katika mashindano ya dunia ya Aquatics ya mwaka 2017 alishinda medali ya shaba, ambayo yalikua mafanikio yake ya kwanza makubwa ya Kimataifa[4]. Siku iliyofuata alishinda medali ya fedha katika mashindano hayo[5].

Katika Mashindano ya Dunia ya Aquatics mnamo Julai 2019 yeye na kundi lake akiwa na Vladislava Alekseeva, Yana Narizhna, Kateryna Reznik, Anastasia Savchuk, Marta Fedina, Alina Shinkarenko na Elizaveta Yakhno walishinda tuzo za shaba.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-12-06. Iliwekwa mnamo 2021-12-06. 
  2. http://www.omegatiming.com/File/Download?id=0001110300FFFFFFFFFFFFFFFFFFFF03
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-05-17. Iliwekwa mnamo 2021-12-06. 
  4. http://www.unn.com.ua/uk/news/1677738-ukrainski-synkhronistky-zdobuly-piatu-bronzu-na-chs-v-uhorshchyni
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-12. Iliwekwa mnamo 2021-12-06.