Majadiliano:Abrahamu, Ethnus, Akrates, Yakobo na Yohane

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nina wasiwasi kidogo kuhusu hao. Maana nikiangalia The book of the saints of the Ethiopian church, namkuta Abrahamu kwa kirefu kidogo uk 1191 lakini tarehe 9 Agosti (V Nahase ya kalenda ya Ethiopia, lakini sijui kama inaweza kutafsiriwa kwa namna mbalimbali), pamoja na Yohane askari (John the soldier) halafu mmoja Filipo wa Dabra Bizan. Ila majina ya Ethnus, Akrates, Yakobo sioni hapa.

Akrates wa Dameski na Yakobo wa Misri wako pamoja tar XVII Manase (kama 21 Agosti?); labda ni hao? Maana hapa naona tena majina ya mmoja Abrahamu na mmoja Yohane waliokufa pamoja na Yakobo. Na Akrates anatajwa kama ndugu wa Entawos (Entaeus) labda huyu "Ethnus" wa makala ya Kiingereza?

Kwa namna yoyote naona tutaje vyanzo vyetu katika makala. Kama vyanzo viko, tafadhali tuvitaje hata hapa swwiki. Kipala (majadiliano) 14:38, 15 Desemba 2019 (UTC)[jibu]

Ndugu, ukurasa huu umetokana na Wikipedia ya Kiingereza, ambayo inasema vilevile kwamba hakuna habari zaidi za kihistoria, ila wanaheshimiwa na Waethiopia. Hiyo taarifa ni ya kweli na inathibitishwa na kalenda yao. Hatudaiwi kufanya hivyo sisi pia. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:55, 16 Desemba 2019 (UTC)[jibu]
Umefanya vizuri kutoa maswali yako katika toleo la Kiingereza. Labda tutapata mwanga. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:01, 16 Desemba 2019 (UTC)[jibu]
Nadhani tatizo hapa ni makala nyingi za watakatifu hao (kutoka nchi ambazo ni geni au mabli kwa mtazamo wa Ulaya au Marekani) zina msingi hafifu; najua kamusi kubwa za watakatifu ambazo zinatumia utaalamu mkuu, lakini vitabu vingine vimetungwa tu na watu wanaopenda mada (kidogo kama kwetu wikipedia) na katika vitabu vya kawaida hawapaswi kuonyesha vyanzo kwa kila kipengele. Kwa hiyo kama anaandika kuhusu historia ambayo si ya kwake, makosa yanaingia haraka, ni vigumu kuyatambua. Kumbe tunapata chanzo kinachokubaliwa katika wikipedia inayonakiliwa kote. Hivyo ndivyo jisi iivyo. Kipala (majadiliano) 09:37, 16 Desemba 2019 (UTC)[jibu]
Pengine ni kama kurasa juu ya miungu ya Ugiriki: sisi hatuiamini, lakini tunaeleza watu waliweza kuiabudu, tena siku hizi wanarudi kuiabudu kwa kuacha Ukristo. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:41, 16 Desemba 2019 (UTC)[jibu]