Kingbaka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kingbaka ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumzwa na Wangbaka. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kingbaka imehesabiwa kuwa watu zaidi ya milioni moja. Pia kuna wasemaji 3000 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na 3650 nchini Jamhuri ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingbaka kiko katika kundi la Kiadamawa-Ubangi.

Viungo vya nje [hariri]

Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.