Kidole gumba
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kidole gumba ni kidole cha kwanza mkononi. Kidole hiki ni tofauti na vidole vingine kwa sababu mwelekeo wake ni wa pekee. Kina viungo vichache pia ni kifupi. Kinatuwezesha kushika vitu.
Katika tamaduni mbalimbali kuonyesha kidole gumba kuna maana ya furaha; kwa mfano kumkubali mtu, kumwambia: Umefanya vizuri au pia kumwonyesha: mimi sijambo, sina matata.