Kiganja
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kiganja (pia: kitengele) ni sehemu ya mwisho wa mkono inayoishia kwa vidole. Inaunganishwa kwa kiwiko na kigasha. Binadamu huwa na viganja viwili, kila kimoja huwa kwa kawaida na vidole 5. Mtu hutumia kiganja na vidole kwa kushika vitu na kutumia vifaa vingi.
Sehemu ya ndani ya kiganja ni kofi.
Mtu akikunja vidole pamoja na kiganja ngumi (sumbwi) inapatikana inayotumiwa kwa kupiga kwa ukali kwa mfano wakati wa mchezo wa ngumi.
Tazama pia [hariri]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: