Kibengali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kibengali (বাংলা ভাষা Bāṃlā bhāṣā, Bangla bhasha) ni lugha ya Asia ya Kusini inayojadiliwa katika Bangladesh na India. Jumla ya wasemaji ni takriban milioni 230. Ni lugha ya taifa ya Bangladesh na upande wa Uhindi ni lugha ya jimbo la Bengal Magharibi. Kati ya lugha za Uhindi zenye wasemaji wengi ni lugha ya pili. Inahesabiwa kuwa lugha ya dunia yenye wasemaji wengi ya tano au sita.

Kinahesabiwa kuwa kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi ndani ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Lugha za karibu ni pamoja na Kihindi, Kiurdu, Kipunjabi, Kisindhi, Kigujarati na Kimarathi.

Ni lugha yenye fasihi tangu miaka 1,000. Mwandishi Rabindranath Tagore aliyeandika kwa Kibengali alipokea Tuzo ya Nobel ya Fasihi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kibengali kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.