Kibelait

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kibelait ni lugha ya Kiaustronesia nchini Brunei na Malaysia inayozungumzwa na Wabelait. Idadi ya wasemaji wa Kibelait nchini Brunei imehesabiwa kuwa watu 1000; idadi nchini Malaysia haijulikani. Kwa vile Wabelait wengi wameanza kuacha lugha yao na kutumia Kimalay ya Brunei badala yake, Kibelait imekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibelait iko katika kundi la Kiborneo-Kaskazini.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kibelait kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.